Habari za Punde

Mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya Zimamoto na Jangombe Boys Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Timu ya Zimamoto Imeshinda Bao 3-2.

Mchezaji wa Timu ya Jangombe Boys  na Zimamoto wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedong jana.Timu ya Zimamoto imetoka kifua mbele kwa ushindi wa Bao  3-2.

MAAFANDE wa timu za Polisi, Mafunzo na Zimamoto wametoka kidedea katika michezo yao ya ligi kuu ya Zanzibar iliyochezwa jana kwenye viwanja viwili tofauti.

Polisi iloshuka katika dimba la Gombani iliifunga Selem View bao 1-0, wakati Zimamoto imeifunga Jang'ombe Boy's mabao 3-2 na Mafunzo iliwafunga Jamhuri mabao 4-0.

Polisi katika mchezo huo bao lake lilifungwa na Suleiman Nuhu, wakati Mafunzo mabao yake mawili yalifungwa na Paulo Godfrey na Daudi Jesca Madata na Rashid Abdalla Gaspa walifunga bao moja kila mmoja.

Kwa upande wa timu ya Zimamoto ambao mchezo wao ulichezwa uwanja wa Mao Dze Dong  mabao yake yalifungwa na Hafidh Barik dakika ya 10 na 27 na Khalid Kheri dakika ya 75, wakati Boy's mabao yao ya kufutia machozi yalifungwa na Abdulkarim Naimu dakika ya 72 na Khatibu Ameir Khatib dakika 86.

Hata hivyo Zimamoto inayofundishwa na Hassan Abrahman watajilaumu mno kutokana na kukosa nafasi nyingi za wazi hasa katika kipindi cha kwanza.

Kwa matokeo ya michezo hayo Polio imefikisha pointi 32 na kupanda hadi nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi hiyo kutoka nafasi ya nane na Mafunzo wamefikisha pointi 31 na kuendelea kubakia katika nafasi yake ya tisa.

Wakati Zimamoto ambao mchezo wao ulihudhuriwa na mashabiki kocha ya Serikali kupiga marufuku wamefikisha pointi 45 na kupaa hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na KMKM.

Ligi hiyo Leo itaendelea tena kwa kupigwa michezo miwili ambapo katika uwanja wa Mao Dze Dong JKU itapambana na KMKM na Gombani Chipukizi itakwaruzana na Machomanne.
Mshambuliaji wa Timu ya Jangombe Boys akimpita beki wa Timu ya Zimamoto wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar.Timu ya Zimamoto imeshinda bao 3-2.
Beki wa Timu ya Zimamoto akijaribu kumzuiya mshambuliaji wa Timu ya Jangombe Boys akiwa na mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar.
Benchi la Ufundi la Timu ya Jangombe Boys wakifuatilia mchezo wao wac Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar.Timu Jangombe Boys imesalim amri kwa kufungwa bao 3-2.
Wachezaji wa Timu ya Zimamoto na Jangombe Boys wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar Timu ya Zimamoto imeshinda bao 3-2.
Wachezaji wa Timu ya Jangombe Boys wakimlalamikia muamuzi wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika katika Uwanja wac Mao Zedong Jijinin Zanzibar.
Mshika kibendera akiwa ameinua kibendera juu kuashiria kuotea kwa mchezaji wa Timu ya Jangombe Boys, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedong jana Timu ya Zimamoto imeshinda mchezo huo kwa bao 3-2.
Kizaazaa katika goli la Timu ya Zimamoto 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.