Habari za Punde

MKUU WA JESHI LA ANGA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUBUNI MIFUMO YA USIMAMIZI WA FEDHA

Mchumi Bw. Elihudi Yessaya, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la Anga Meja Jenerali George William Ingram, kuhusu mkakati wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 katika kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, alipotembelea banda la wizara na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
 Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Juma Mfaume akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la Anga Meja Generali George William Ingram, kuhusu mchakato wa uandaaji, uwasilishaji, utekelezaji na usimamizi wa Bajeti ya Serikali katika kufanikisha kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, alipotembelea Banda la Wizara hiyo  pamoja na Taasisi zake wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya 44 ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Maendaenda, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la Anga Meja Jenerali George William Ingram, kuhusu Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) wenye lengo la kuongeza uwazi na udhibiti wa fedha za umma, kuboresha na kurahisisha namna ya kulipia huduma za Umma, katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Jeshi la Anga Meja Jenerali George William Ingram, akisikiliza maelezo ya Mfumo mpya wa Manunuzi ya Umma kwa njia ya Mtandao (TANEPS) kutoka kwa Msimamizi wa Mifumo ya Habari wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Giftness David, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Arusha Bi. Sarah Goroi, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la Anga Meja Jenerali George William Ingram, kuhusu kozi mpya zinazotarajiwa kuanza kufundishwa na chuo hicho mwezi Oktoba, 2020 wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.