Habari za Punde

Mwenyekiti wa UVCCM Wilayani Handeni Awania Kiti cha Ubunge Jimbo la Handeji Mjini.Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Handeni  Mkoani Taanga Ndg. Ahmad Chihumpu akirejesha Fomu yake ya kuwania kuchaguliwa kupeperusha bendera ya CCM, akikabidhi kwa Katibu wa UWT Wilaya  Bi.Aisha Mpuya.

Na Hamida Kamchalla, HANDENI.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Ahmadi Chihumpu jana alirudisha fomu yake ya kuwania kiti cha Ubunge katika Jimbo la Handeni mjini na kusema kuwa nia ya kuwania nafasi hiyo ni kutaka kurudisha heshima ya chama chake ndani ya Jimbo hilo.

Chihumpu alieleza kwamba pamoja named nia yake hiyo pia kilichomsukuma zaidi ni kuwatumikia wananchi wa Handeni mjini katika mambo matatu ambayo yamekuwa changamoto kubwa isiyopatiwa ufumbuzi ndani ya vipindi vyote vya uongozi uliopita.

"Kilichonisukuma nichukue fomu hii ni mambo mawili, kwanza kurudisha heshima ya chama changu ndani ya jimbo na pili ni kutwaka kuwatumikia wananchi wa Handeni katika kutatua changamoto sugu ambazo zinasumbua miaka yote, nitajikita zaidi katika kutatua kero ya afya, elimu na miundombinu hususani katika sekta ya maji" alisema Chihumpu.

Aidha alisema kuwa mbali na hayo zaidi amevutiwa sana na utendaji wa Rais John Magufuli ambaye kwa kiasi kikubwa amechangia mwaka huu vijana wengi kujitokeza na kutia nia za kugombea nafasi mbalimbali ambazo awali zilibanwa na kuwafanya wakose uwezo wa kuziwania.

"Pamoja na yote nimpongeze sana Rais wetu Magufuli kwa kuona vijana na watu wanyonge wenye hali ya chini tuna umuhimu na haki ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini mwetu kwani awali nafasi hizi zilikuwa zinawaniwa na watu wenye uwezo wa kifedha tuu ilihali wapo watu wenye uhitaji na uwezo lakini hawakuwa na fedha za kuchukulia fomu" alieleza.

Chihumpu alifafanua kwamba awali fomu za kugombea nafasi ya Ubunge zilikuwa zinatolewa kwa kiasi cha kuanzia shilingi milioni 3.5 hadi 5 lakini Rais amelifanya suala hilo kutoka katika kiwango hicho hadi shilingi laki 1 kwa mwaka huu wa uchaguzi.

Hata hivyo Chihumpu alibainisha kipaumbele chake kuwa ni kuinua michezo ndani ya Wilaya hiyo ambayo kwasasa hakuna timu ya kueleweka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.