Habari za Punde

Wazazi na Walezi Watakiwa Kutakata Tamaa za Kimaisha Watakiwa Kupambana Kuona Haki Itendeka.

Mtalamu wa saikolojia kutoka chuo cha afya Zanzibar Asya Saleh Abdukatif akifafanua jambo juu ya umuhimu wa jamii kutokata tamaa.
Afisa utafiti na ufuatiliaji TAMWA-Zanzibar Mohamed Khatib akifafanua jambo juu ya umuhimu wa jamii kutoa ushahidi dhidi ya kesi za udhalilishaji.
Baadhi ya washiriki wa kujengewa uwezo juu ya kutoa ushahid dhidi ya kesi mbali mbali za udhalilishaji kwa wanawake na watoto Zanzibar.
Wakili kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) Khamis Juma akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa ushahidi uliokamilika katika kesi za udhalilishaji.

Na.Muhammed Khamis,TAMWA-Zanzibar

Jamii visiwani Zanzibar imetakiwa kutokata tamaa iwapo ndani ya familia zao kuna baadhi ya watoto wamefanyiwa matendo ya udhalilishaji wa kijinsia na kujihisi hawana haki ya kuishi kama wanavoishi wengine.



Ushauri huo umetolewa na mtalamu wa saikojia kutoka chuo kikuu cha Afya Zanzibar (ZSH) Bi.Asya Saleh Abdulatif wakati alipokua akizungumza na baadhi ya wazazi ambao watototo wao wamewahi kufanyiwa matendo hayo katika ukumbi wa TAMWA-Zanzibar Tunguu wilaya ya kati Unguja.



Alisema wazazi ama walezi hawapaswi kujilaumu wala kukata tamaa mara baada ya watoto wao wanapotendewa matendo hayo na kueleza kuwa wanapaswa kupambana kuona haki inatendeka.



Alieleza kuwa kikawaida watu wengi huathirika kisaikolojia na kushindwa kufanya lolote ikiwemo kukata tamaa za kimaisha na kupekekea kushidnwa kutimiza ndoto zao.



Alisema ili wazazi ama walezi kuweza kuepuka changamoto za kuchanganyokiwa kisaikolojia hawana budi kushirikisha wengine matatizo yao na kuepuka kabisa kunyamazia maovu.



Hata hivyo mtalamu huyo wa saikolojia aliwaasa wazazi hao kutofanya maamuzi ya haraka mara wanapokutana na mazingira ya aina hio badala yake watumie muda mwingi kutafakari. 



Awali afisa kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka Khamis Juma alisema wazazi wanapaswa kuhakikisha wanatoa mashirikiano kikamilifu katika kutoa ushahidi dhidi ya kesi za udhalilishaji.



Hata hivyo alisema wazazi wasikubali kutishwa kwa kulazimishwa kuleta idadi kubwa ya mashahidi badala yake hata mtu mmoja ikiwemo mfanywaji wa tendo la udhalilishaji pekee unatosha.



‘’Muhimu ni kujiridhisha anachokisema shahidi ni ukweli uliojiridhisha bila ya chembe ya hofu’’aliongezea.



  Hata hivyo aliwataka wazazi kuhakikisha wanawatengezea mazingira mazuri watoto wao kwa lengo la kutoa ushahidi wenye kujitosheleza kabisa mahakamni ili watendaji wa hayo waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sharia.



Aidha wakakili huyo alisema ili yote yaweze kutendeka na mshtakiwa kuchukuliwa hatua ni lazima mashahidi wafike Mahakamani kutoa ushahidi na si vyenginevyo.



Nae Aboud Rajab mkaazi wa shehia ya Muyuni kusini Unguja ambae ni miongoni ma wazazi ambao mtoto wake alipata kufanyiwa udhalilishaji wa kijinsia alisema kuna changamoto katika vyombo mbali mbali vya sharia.



Alisema hadi sasa yeye binafsi ni mwaka wa pili kesi yake iko Mahakamani bila kutolewa huku na kuambiw akuwa mshtakiwa amewekwa rumande kwa miaka miwili bila ya kupewa hukumu. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.