Habari za Punde

TAARIFA YA TANESCO KUHUSU MATENGENEZO KINGA KATIKA VITUO VYA KUPOZA UMEME VYA MLANDIZI NA CHALINZE.Na mwandishi wetu.
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wa Mkoa wa Pwani kuwa kutakuwa na maboresho katika miundombinu ya Vituo vya kupoza umeme vya Mlandizi na Chalinze msongo wa umeme kilovoti 132/33.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu imesema ratiba ya kazi itafanyika kuanzia leo Jumatatu Julai 20, 2020 kuanzia Saa 02:30 Asubuhi hadi Saa 12:00 Jioni ambapo Kituo cha Mlandizi chenye msongo wa umeme wa kilovolti 132 kitazimwa ili kuruhusu mafundi wa TANESCO kufanya matengenezo kinga ya mwaka kwenye miundo mbinu ya kituo.

Taarifa imetaja maeneo yatakayoathirika ni pamoja na Wateja wote wanaopata umeme kutoka Kituo cha Mlandizi ambao ni Mlandizi, Visiga, Kongowe, Picha ya ndege, Ruvu, Vigwaza na Viwanda vya Hong-Yu pamoja na Kiluwa.

Aidha taarifa imesema siku ya Jumanne Julai 21, 2020 kuanzia Saa 02:30 Asubuhi hadi Saa 07:00 Mchana, "Busbar" namba moja yenye msongo wa umeme wa kilovolti 33 itazimwa ili kuruhusu mafundi wa TANESCO kufanya matengenezo kinga ya mwaka kwenye miundombinu ya msongo wa umeme wa kilovoti 33 ambayo ni maeneo ya Viwanda vya Hong-Yu pamoja na Kiluwa kuanzia Saa 08:00 mchana hadi Saa 12:00 jioni  "busbar" namba mbili yenye msongo wa umeme wa kilovolti 33 itazimwa ili kuruhusu mafundi wa TANESCO kufanya matengenezo kinga ya mwaka kwenye miundombinu ya msongo wa umeme wa kilovoti 33.

Maeneo yatakayoathirika na hatua hiyo ni pamoja na baadhi ya wateja wanaolishwa na kituo cha Mlandizi ambao ni Mlandizi, Visiga, Kongowe, Picha ya ndege, Ruvu na Vigwaza.

Wakati siku ya Jumatano Julai 22, 2020 kuanzia Saa 02:30 Asubuhi hadi Saa 12:00 Jioni, Kituo cha Chalinze chenye msongo wa umeme wa kilovolti 132 kitazimwa ili kuruhusu mafundi wa Tanesco kufanya matengenezo kinga ya mwaka kwenye miundo mbinu ya kituo.
“Maeneo yatakayoathirtika ni wateja wote wanaolishwa na kituo cha Chalinze ambao ni Ruvu juu, Ngerengere, Ubena na viwanda vya Keda pamoja na Sayona.

Aidha TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.