Habari za Punde

Wagombea Uongozi Watakiwa Kujiepusha na Rushwa Katika Mchakato wa Uchaguzi

Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA) imesema itaendelea kutoa elimu kwa Wananchi,Taasisi za Serikali na Binafsi ili kuepusha Rushwa hasa katika kipindi hiki cha kueleka katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2020.
Wito huo umetolewa huko Mwera Wilaya ya Magharibi ‘’A’’na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma kutoaka ZAECA Bw. Sheha Kombo Hamad wakati wa majumuisho ya utoaji wa elimu ya kukabiliana na Maafa kwa Majimbo ya Mkoa wa Magharibi kichama.
Amesema Chama cha Mapinduzi kimeweka Utaratibu maalum wa kuwapata Viongozi wake hivyo hakitoweza kuwafumbia Macho watakaobainika kupokea au kuchukuwa Rushwa.
Aidha amesema Serikali imeweka Mikakati na Mipango mbalimbali ya kukabiliana na suala hilo kwani ni Aduwi wa haki na inarudisha nyuma maendeleo ya Mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla.
Kwa Upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Bw. Mgeni Mussa Haji amesema wameandaa Mafunzo kwa Kamati za Siasa katika Majimbo,Wadi na Matawi katika Mkoa huo ili wazidi kupata uelewa wa kujikinga na Utumiaji wa Rushwa katika maeneo yao.
Aidha Katibu huyo ameiomba ZAECA kufuatilia Mwenendo wa Rushwa kwa Vyama vyengine na sio kuegemea Chama cha Mapinduzi pekee kwani navyo ni sehemu katika jamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.