Habari za Punde

WAKUU WA VIKOSI VYA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR (SMZ) WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI JIJINI DODOMA.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga (Kulia), akisalimiana na Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar, Ali Malimussy (kushoto), baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma.

Wakuu wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wakiongozwa na Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar, Ali Malimussy watembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini yaliyopo jijini Dodoma. Lengo ni kukuza mahusiano na ushirikiano kati ya vyombo hivyo.

Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga, alitumia fursa hiyo kuwapongeza Wakuu wa Vikosi hivyo kwa kazi nzuri wanazozifanya na kuwaahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa.

Aidha Kamishna Malimussy amemshukuru CGF John Masunga kwa niaba ya Ujumbe uliotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo. “Tumejifunza mengi lakini pia tunashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona jinsi gani tunaweza kushirikiana” alisema Kamishna Malimussy.
Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar Ali Malimussy, akisaini kitabu cha wageni wakati walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma, akiwa ameambatana na Wakuu wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), lengo ni kukuza mahusiano na ushirikiano kati ya vyombo hivyo, (Kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga.
Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar Ali Malimussy, akifafanua jambo, wakati walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma akiwa ameambatana na Wakuu wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) mapema leo.
Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Ali Ali (kulia), akimshukuru Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga kwa niaba ya Ujumbe uliotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo jijini Dodoma mapema leo.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna wa Kikosi cha  Zimamoto na Uokozi Zanzibar, Ali Malimussy (Wanne kutoka kushoto), Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Ali Ali (Watatu kutoka kushoto), Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) Ali hamad ( Wasita kutoka kulia), Wajumbe toka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo wakati walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma mapema leo.
(PICHA NA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.