Habari za Punde

VIJANA WA JESHI LA AKIBA MOSHI DC "KUPIGWA MSASA" NA VYOMBO VYA USALAMA

Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kundi la 50 kwa jeshi la akiba wilaya ya Moshi vijijini ,Katibu tawala msaidizi Nathanieli Mshana akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo.

Na Dixon Busagaga ,Moshi 
IDARA za serikali zikiwemo Jeshi la Polisi ,Usalama wa Taifa ,Taasisi ya kuzia na kupambana na Rushwa nchni (TAKUKURU) pamoja na Jeshi la zima moto na uokoaji zimetajwa kuhusika katika mafunzo kwa kundi la 50 la vijana wanaojiunga na jeshi la akiba katika wilaya ya Moshi.

Uzalendo ,Uzalendo,Uzalendo ni maneno ambayo yamekuwa yakihubiriwa kwa kundi la vijana yakilenga kundi hili kujitoa kwa ajili ya nchi yao kama inavyoonekana kwa vijana hawa waliojitolea kujiunga na jeshi la akiba.

Vijana 111 kutoka tarafa ya Kibosho katika wilaya ya Moshi miongoni mwao 97 wakiwa ni wanaume na 14 wakiwa ni wanawake wameanza mafunzo yatakayodumu kwa zaidi ya majuma 18 kama anavyoeleleza Kepteni Hansi Mwakanyamale ,kiongozi wa mafunzo hayo.

“Vijana waliojitolea kujiunga na jeshi la akiba ,mafunzo yataendeshwa kwa majuma 18,masomo watakayo jifunza ni nadharia na vitendo yakiwemo masomo ya Kwata,Uraia ,Usomaji wa ramani ,Mbinu za kivita ,ujanja wa porini,huduma za kwanza .silaha ,sharia za jeshi ,muundo wa jeshi ,utimamu wa mwili ,uhandisi wa medani ,mapigano ya singe ,vita msituni ,uzalendo na usalama wa raia”alisema Kepteni Mwakanyamale.

Alisema mmani ya jeshi la akiba wilaya ya Moshi ni kuhakikisha kwamba mkaazi wa wilaya hiyo atakayehudhuria na kufaulu mafunzo hayo anakua ni tegemeo la nchi na kiusalama kwa watanzania wote na kwamba anakua ni tegemeo la watanzania wengine ambao hawajapata nafasi ya kufanya mafunzo hayo.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo Katibu tawala msaidizi Nathanieli Mshana alisema vijan hao wameonesha uzalendo kwa nchi yao na kwamba mafunzo haya yatasaidia kuwajengea ukakamavu na ujasili mkubwa miongoni mwa vijana wengine .

Hili ni kundi la 50 la vijana walioamua kujiunga na mafunzo katika jeshi la akiba katika wilaya ya Moshi ,mafunzo ambayo yamekuwa msaada hasa kwa vijana kwa kuwajengea uzalendo na ukakamavu.
Baadhi ya Viongozi wa jeshi na askari wakiwa na mgeni rasmi katibu tawala msaidizi wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa mafunzo kwa vijana 111 na waliojiunga na jeshi la akiba.
Kiongozi wa Mafunzo kwa vijana waliojiunga na jeshi la akiba katika wilaya ya Moshi ,Kepteni Hansi Mwakanyamale akitoa taarifa kuhusu mafunzo ya kundi la 50 la askari wa jeshi la akiba katika wilaya ya Moshi vijijini.
Baadhi ya vijana kutoka tarafa ya Kibosho waliojiunga na jeshi la akiba wakiwa kwenye maandalizi ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Vijana kutoka tarafa ya Kibosho wakiimba nyimbo mbalimbali wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo kwa kundi hilo la 50 .

Na Dixon Busagaga ,Moshi 

IDARA za serikali zikiwemo Jeshi la Polisi ,Usalama wa Taifa ,Taasisi ya kuzia na kupambana na Rushwa nchni (TAKUKURU) pamoja na Jeshi la zima moto na uokoaji zimetajwa kuhusika katika mafunzo kwa kundi la 50 la vijana wanaojiunga na jeshi la akiba katika wilaya ya Moshi.

Uzalendo ,Uzalendo,Uzalendo ni maneno ambayo yamekuwa yakihubiriwa kwa kundi la vijana yakilenga kundi hili kujitoa kwa ajili ya nchi yao kama inavyoonekana kwa vijana hawa waliojitolea kujiunga na jeshi la akiba.

Vijana 111 kutoka tarafa ya Kibosho katika wilaya ya Moshi miongoni mwao 97 wakiwa ni wanaume na 14 wakiwa ni wanawake wameanza mafunzo yatakayodumu kwa zaidi ya majuma 18 kama anavyoeleleza Kepteni Hansi Mwakanyamale ,kiongozi wa mafunzo hayo.

“Vijana waliojitolea kujiunga na jeshi la akiba ,mafunzo yataendeshwa kwa majuma 18,masomo watakayo jifunza ni nadharia na vitendo yakiwemo masomo ya Kwata,Uraia ,Usomaji wa ramani ,Mbinu za kivita ,ujanja wa porini,huduma za kwanza .silaha ,sharia za jeshi ,muundo wa jeshi ,utimamu wa mwili ,uhandisi wa medani ,mapigano ya singe ,vita msituni ,uzalendo na usalama wa raia”alisema Kepteni Mwakanyamale.

Alisema mmani ya jeshi la akiba wilaya ya Moshi ni kuhakikisha kwamba mkaazi wa wilaya hiyo atakayehudhuria na kufaulu mafunzo hayo anakua ni tegemeo la nchi na kiusalama kwa watanzania wote na kwamba anakua ni tegemeo la watanzania wengine ambao hawajapata nafasi ya kufanya mafunzo hayo.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo Katibu tawala msaidizi Nathanieli Mshana alisema vijan hao wameonesha uzalendo kwa nchi yao na kwamba mafunzo haya yatasaidia kuwajengea ukakamavu na ujasili mkubwa miongoni mwa vijana wengine .

Hili ni kundi la 50 la vijana walioamua kujiunga na mafunzo katika jeshi la akiba katika wilaya ya Moshi ,mafunzo ambayo yamekuwa msaada hasa kwa vijana kwa kuwajengea uzalendo na ukakamavu.

MWISHO

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.