Habari za Punde

Wajumbe Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi watakiwa kuteua madiwani waadilifu

Na Takdir Suweid, Mkoa wa Mjini Magharibi.                                                  
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi wametakiwa kuteua Madiwani Waadilifu watakaoweza kupeperusha Bendera ya Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu na kukipatia ushindi.
Akizungumza katika kikao cha uteuzi wa Wagombea Udiwani wa Majimbo na Viti maalum Mkoa wa Magharibi,Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi katika Mkoa huo Muhammed Rajab Soud huko katika Hoteli ya Sea View Mazizini amesema baadhi ya Madiwani wanapoingia Madarakani wanajishirikisha na migogoro ya ardhi jambo ambalo linapunguza Ufanisi katika Utendaji.
Amesema Viongozi wanatakiwa kuwa Wazalendo na wenye moyo wa kuwatumikia Wananchi na kuepuka migogoro katika jamii.
Amesema ni vyema kuzingatia maamuzi sahihi ya Viongozi hao ili kupatikana kuweza kupatikana Viongozi watakaoweza kufanikisha kupatikana ushindi Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu.
Aidha amewataka kuchagua Viongozi wenye kufuata utaratibu na sheria za chama na kuacha kuchaguwa Viongozi wababaishaji kwa mujibu wa wamilia au urafiki.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Bw. Mgeni Mussa Haji amesema uteuzi huo umezingatia vigezo vinavyokubalika katika Chama na kuwaomba wanachama wa Chama hicho kuwaunga nkono ili kuweza kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi Mkuu.
Kikao cha Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi wameteuwa Madiwani 37 ambapo Wilaya ya Mfenesini 14,Dimani 12 na viti maalum 11

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.