Habari za Punde

*KWANINI WATANZANIA TUMEMCHAGUA RAIS MAGUFULI ATUONGOZE TENA 2020?*

Na Emmanuel J. Shilatu

Sifa kuu 3 zinambeba vilivyo Mwamba wa Afrika na jabari wa mageuzi ya kiuchumi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mpaka kufikia hatua Watanzania kuamua mwaka 2020 aendelee kutuongoza.
*A: UADILIFU*
Rais Magufuli amesimamia mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ambapo wanaotuhumiwa kwa ufisadi Papa na ulaji rushwa wamepandishwa Mahakamani
Pia ameimarisha uwajibikaji, uadilifu na uchapa kazi kwa Watumishi wa umma nchini na kusimama kidete kufufua Mashirika ya umma yaliyokuwa taabani. Mfano shirika la ndege, shirika la simu.
Halikadhalika amefanya uchunguzi wa rasilimali za Taifa na kuweka makubaliano mapya kwenye sekta ya madini.
Rais Magufuli amedhibiti madawa ya kulevya na ujangili wa Tembo na Faru ambapo wameongezeka kuashiria kupungua kwa biashara ya nyara za Serikali.
Kwenye upande wa masuala ya kidiplomasia ameimarisha mahusiano mazuri na nchi jirani.
Haijawahi kutokea kwani Rais Magufuli ameweka uwazi wa taarifa na udhibiti wa rasilimali za Taifa.
*B: UZALENDO*
Baada ya Mwalimu Nyerere anayefuatia ni Rais Magufuli kutoa Elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari ambapo Serikali hutumia Tsh. Bilioni 23 kila mwezi kulipia elimu bure.
Uonevu, ubabe, ubaguzi umepungua na ni sahihi kusema Rais Magufuli amepunguza uwepo wa matabaka ndani ya jamii.
Ni wazo la Mwalimu Nyerere lakini Rais Magufuli amekuja kulitekeleza la ujenzi wa mradi mkubwa wa Mto Rufiji wa kuzalisha umeme zaidi ya Megawatts 2115.
Rais Magufuli amefanikiwa kudhibiti matumizi ya hovyo ya fedha na fedha kuelekezwa zaidi kwenye miradi ya kimaendeleo.
Pia Rais Magufuli yupo imara na amesimamia  ukusanyaji na matumizi sahihi ya kodi. Makusanyo yameongezeka kutoka Tsh. Bilioni 800 hadi kufikia Tsh. Trilioni 1.9 kwa kila mwezi.
Waliojipenyeza kwenye ajira Serikalini bila ya sifa amewaondoa. Hivyo JPM amefanikiwa kudhibiti vyeti feki na mishahara hewa na kubaki historia nchini.
Leo hii Watanzania tunajivunia nchi yetu, viongozi wetu, rasilimali zetu na utaifa wetu. Hivyo JPM Ameimarisha UZALENDO nchini.
Hakuishia hapo amerudisha mashamba na viwanda vilivyobinafsishwa na havikuendelezwa.
Leo Taifa linanufaika na madini kwani amedhibiti usafirishwaji wa makinikia na hayaendi kuchenjuliwa tena nje na madini yanauzwa hapa hapa nchini kupitia masoko ya madini yaliyoanzisha maeneo mbalimbali yenye madini. Huu ni uzalendo wa kuigwa wenye tija vizazi na vizazi.
*C: UCHAPA KAZI*
Leo hii Serikali imehamia Dodoma na mpaka Rais Magufuli nae pia amehamia Dodoma. Walisema haiwezekani lakini nia ya dhati na uchapa kazi wa Rais Magufuli na Serikali yake imedhihirisha inawezekana.
Baada ya reli ya Mkoloni yenye zaidi ya miaka 120, leo hii Rais Magufuli ameanzisha Ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme ya SGR ambayo ni reli ya kisasa, yenye kasi na inayobeba mizigo mingi.
Sera ya Tanzania ya viwanda ipo kivitendo. Leo hii kuna ujenzi wa viwanda vipya zaidi ya 3000.
Rais Magufuli aliapa kuilinda katiba ya nchi ambapo kuna uimarishwaji wa amani na Uhuru wa kidemokrasia ndani ya nchi. Mathalani Umoja wa Mataifa (UN) umempongeza Rais Magufuli kudumisha amani na usalama ndani  na nje ya nchi.
JPM amesimamia vyema ukuaji wa uchumi uliokuwa na kufikia 7.1%
Kwenye afya napo pamenoga kuna ujenzi wa vituo vya afya kila kata na ujenzi wa Zahanati kila kijiji.
Serikali ya Rais Magufuli imedhibiti maandamano ya kisiasa na ya kijamii (Mf. Wanafunzi, Madaktari) na sasa yamebaki historia.

JPM amenunua ndege mpya 8 za kisasa na Leo hii ATCL imefufuka inachanja anga za kitaifa na kimataifa.
Ameweka mikakati mizito ya kupunguza foleni kwa Ujenzi wa flyover ya Tazara na interchange ya Ubungo.
0767488622

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.