Habari za Punde

MENEJIMENTI YA OFISI YA WAZIRI MKUU YAPATIWA MAFUNZO YA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA

fisa Ununuzi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Frank Yesaya akitoa mafunzo kwa Wakurugenzi wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma pamoja na kanuni zake katika ukumbi wa mikutano uliopo jengo la PSSSF, Jijini Dodoma.


Na. Mwandishi Wetu, OWM – KVAU

Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imepatiwa mafunzo na Wataalamu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya mwaka 2011 na mabadiliko yake ya mwaka 2016 ili kuwajengea uwezo zaidi katika suala la ununuzi na kusimamia mikataba ya ununuzi wa umma pamoja na kuhakikisha mikataba inayoingia baina ya Ofisi na Wazabuni haileti kasoro yoyote.

Mafunzo hayo yamefanyika hii leo Oktoba 20, 2020 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la PSSSF, Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.