Habari za Punde

Utiaji saini wa mnakabidhiano ya miradi ya ZUSP wafanyika

Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa (kushoto)akitiliana na Saini na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri kuhusiana na Makabibidhiano ya Miradi ya Mbalimbali ya ZUSP hafla iliofanyika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga Mjini Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa (kushoto) akikabidhiana hati ya saini  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri kuhusiana na Makabidhiano ya Miradi ya Mbalimbali ya ZUSP hafla iliofanyika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga Mjini Zanzibar.

Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa (kushoto)akikabidhiana Funguo za Buldoza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri kuhusiana na Makabibidhiano ya Miradi ya Mbalimbali ya ZUSP hafla iliofanyika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga Mjini Zanzibar.

 Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwaa akitoa hotuba baada ya kutiliana saini na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri kuhusu Makabibidhiano ya Miradi ya Mbalimbali ya ZUSP hafla iliofanyika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga Mjini Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri akitoa hotuba baada ya kutiliana saini na Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa kuhusu Makabibidhiano ya Miradi ya Mbalimbali ya ZUSP hafla iliofanyika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Vuga Mjini Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA/MAELEZO ZANZIBAR

 a Maryam Kidiko/Maelezo.           

Wizara ya Fedha na Mipango imekabidhi Miradi ya Ujenzi wa Misingi ya Maji ya Mvua  kwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa,  Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ baada ya kukamilika kwake.

Akikabidhi miradi hiyo katika ukumbi wa Wizara hiyo Waziri wa Fedha na Mipango  Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa amesema miradi hiyo ina lengo la kupunguza mafuriko wakati wa mvua katika maeneo mbalimbali ya mjini.

Amsema miradi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza maafa ya mvua katika kipindi cha masika kutokana na misingi yote kuweza kufanya kazi vizuri.

“ Mradi huo umeleta mafanikio makubwa tofauti na hapo mwanzo kwani maeneo mbali mbali yameweza kuwa na miundo mbinu bora katika makaazi yao”, ameeleza Waziri huyo.

Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  imetumia gharama kubwa za kujenga miundo mbinu bora ili Wananchi waweze kuishi katika mazingira mazuri nchini.

Amefahamisha kuwa misingi hiyo inatumika kutoa huduma kwa jamii lazima ituzwe ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kutimiza lengo lililokusudiwa .

Miradi ya Ujenzi wa misingi ya maji ya mvua yenye urefu wa mita 20,400 (20.4km) imehusisha  maeneo ya Karakana, Mnazimmoja, Magomeni, Kwabinti hamrani, Meya, Migombani, Sebleni na Shauri moyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.