Habari za Punde

Mahafali ya 15 ya Skuli ya Lion King Junior Academy

 Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw Omar Ali Omar (Bhai) akitoa nasaha zake katika mahafali ya tano ya skuli ya Lion King Junior Academy
Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw Omar Ali Omar (Bhai) akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao katika mahafali ya kumi na tano ya skuli ya Lion King Junior Academy

 Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw Omar Ali Omar (Bhai) alipokuwa akizungumza na wanafunzi pamoja na wazazi kwenye mahafali ya kumi na tano ya skuli ya Lion King Junior Academy kulia ni mkurugenzi wa Skuli ya Lion King Mahmoud Ibrahim

 Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw Omar Ali Omar (Bhai) amesema Serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi itahakikisha Elimu inatolewa bila ya ubaguzi ili kuweza kuibua vipaji mbali mbali kwa Wanafunzi.

Akizungumza katika mahafali ya Skuli ya Lion King Junior Academy katika ukumbi wa Taasisi Vuga mjini Unguja amesema Elimu ni haki ya kila Mwananchi bila ya kujali kuwa inatolewa kwa Skuli za binafsi au Serikali.
Aidha amewashukuru Walimu kwa jitihada kubwa waliyoionesha kwani wameweza kuongeza idadi ya ufaulu na kufanikiwa kuibua vipaji mbali mbali katika Skuli yao.
Pia Amewataka wazazi kuitenga siku maalum kwenda Skuli ili kuskiliza maendeleo ya watoto wao kwani kufanya hivyo kutawasaidia kuweza kujua maendeleo na mahudhurio ya watoto wao.
Pia Mkurugenzi ameupongeza uongozi wa Skuli kwa kuwa karibu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa kuhakikisha wanapata kibali cha kutoa elimu na kuzitaka Skuli nyenginezo ambazo hazijapatiwa usajili kufanya haraka kusajili ili kuepusha matatizo yasio ya lazima.
Aidha Amesema, Elimu ni zawadi yenye thamani kubwa hivyo amewataka wazee wawekeze elimu kupitia Watoto wao kwani ndio jambo la busara kwa maisha ya watoto wao.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Skuli ya Lion King Junior Academy Ndugu Mahmoud Ibrahim Musallam amewataka Wazazi na walezi kuwahamasisha watoto kuwapenda Walimu na kuwathamini Walimu wao kwani kufanya hivyo kutawasaidia Wanafunzi kujenga mahusiano mazuri na Walimu wao.
Aidha amewataka Wazazi kuacha tabia ya kuwasema vibaya walimu mbele ya watoto wao, Kwani kufanya hivyo ni kumshushia hadhi mwalimu.
Pia amewanasihi Wanafunzi kuwapenda Walimu wao na kuwataka kutokuwa na tabia ya kuwavunjia heshima Walimu wao, kwani kufanya hivyo ni kuivunjia hadhi Elimu watakayo kuja kuitumia baadae.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.