Habari za Punde

Matukio ya Mbalimbali Kuapishwa Kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma 5/11/2020.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa katika gari maalum ya JWTZ wakiwasalimia Wananchi waliofika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuapishwa iliofanyika jana 5/11/2020.  
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono na kuwasalimia Wananchi waliofika katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma kuhudhuria hafla ya kuapishwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi na Rais wa Jamuhuri ya Comoro Mhe. Azali Athuman wakimpungia mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiingia uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma, wakati wa hafla ya kuapishwa ilifanyika jana 5/11/2020.
Marais Wastaaf  wakiwa katika Jukwaa Kuu la Viongozi  wakiwa wamesimama wakati Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, akiingia katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodona jana 5/11/2020.
Wananchi na Wageni waalikwa wakishangilia wakati Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma jana 5/11/2020, wakati wa hafla ya kuapishwa iliofanika katika Uwanja huo.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakitowa Salamu ya heshima kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kuapishwa iliofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma jana 5/11/2020. 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kuapishwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, hafla hiyo imefanyika katika uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma jana 5/11/2020.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.