Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Awasili Jijini Dodoma Kuhudhuria Ufunguzi wa Bunge la 12 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kesho 13/11/2020.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Dkt. Mahenge  Binilith, alipowasili Uwanja wa Dodoma  leo jioni 12/11/2020, kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa Bunge la 12 la  Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika kesho 13/11/2020
RAIS wa Zanzibar na Mwebyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi  akielekea katika ukumbi wa mapumziko baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo jioni 12/11/2020,akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt Mahenge Binilith, kwa ajili ya kuhudhuria Ufunguzi wa Bunge la 12 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hapo kesho 
 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyiamewasili Jijini Dodoma leo kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika uwanja wa ndege wa Dodoma, Rais Dk. Hussein amepokewa na viongozi mbali mbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kulizindua Bunge hilo la 12 mnamo majira ya asubuhi hapo kesho Ijumaa.

Kwa kawaida Mkutano wa Kwanza wa Bunge jipya kama huo huwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analihutubia Bunge kwa maana ya kuweka dira kwenye Serikali yake kwa miaka mitano inayokuja na utekelezaji wa Ilani kadri anavyoona inafaa.

Shughuli hiyo ya uzinduzi wa Bunge itatanguliwa na gwaride maalum ambalo Rais Magufuli atalikagua kabla ya kuingia Bungeni kuhutubi Taifa na kuzindua Bunge.

Rais Magufuli atalihutubia Bunge hilo la 12 ambalo kwa zaidi ya asilimia 90 lina Wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilichoshinda kwa kishindi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28,2020 wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Ambapo kati ya Majimbo 264 ya Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeshinda Majimbo 256 na kina Wabunge wa Viti Maalumu 94.

Katika safari hiyo, Rais Hussein Mwinyi amefuatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.