Na.Himid Choko. BLW
Mkuu wa Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Zanzibar Dkt Yahya Khamis Hamadi amesema Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wana wajibu wa kutambua na kufatilia kero na matatizo ya wananchi na hatimae kuyapatia ufumbuzi kwa lengo la kuleta maendeleo katika majimbo au makundi wanayoyawakilisha.
Akizungumza
katika semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi huko Chukwani , Dkt
Yahya amesema miongoni mwa kazi za mwakilishi
ni kufuatilia miradi ya maendeleo iliyokubaliwa kutekelezwa katika
maeneo yao.
Amesema
katika wajibu kutimiza huo, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hawana budi
kutenga muda wao na kufanya vikao na wananchi wote wa maeneo yao ili kuwapa
fursa wananchi kubadilishana mawazo na uwelewa pamoja na uzoefu kuhusiana na
hali halisi zinazowakabili kwa lengo la kuyapatia ufumbuzi matatizo yako.
Amesema
kwa kutumia rai hiyo, mjumbe anaweza kupata taarifa taarifa zitakazomuwezesha
kujua vipaombele vya wananchi wa eneo lake na kufikisha taarifa hizo kwenye
ngazi zinazohusika na utawala wa nchi kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.
Amesema
kwa misingi hiyo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi lazima aweze kupambanua
usahihi na umuhimu wa mambo yanayodaiwa na wananchi wa eneo lake.
Kuhusiana na Maadili ya Mwakilishi Dkt Yahya amefahamisha kwamba Mjumbe anatakiwa wakati wote kuzingatia maadili ya kazi zake ili pamoja na kulinda heshima ya Baraza na taifa kwa jumla kwa kuhakikisha kuwa hajiingizi katika vitendo vinavyoweza kulidhalilisha Baraza.
Amevitaja
baadhi ya vitendo hivyo ni pamoja na rushwa, kashfa au matumizi ya lugha ya matusi,
mavazi yasiyoheshimu mila, desturi na utamaduni wa Wazanzibari na mambo yanayofanana
na hayo.
Mapema
akitoa mada inayohusiana na Historian a Maendeleo ya Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Mkurugenzi wa Mashtaka ndugu Ibrahim Mzee Ibrahim amesema Maendeleo
makubwa yamepatikana ikiwa ni pamoja na Kuongezeka kwa ushiriki wa wanawake hususan
nafasi maalum kutoka 5 mwaka 1980
hadi kufikia asilimia 40% (nafasi 20 )
hivi sasa na kuongezeka kwa idadi ya wajumbe wawakilishi waliochaguliwa na wananchi
moja kwa moja kutoka wajumbe 10 mwaka 1980 ililipoanzishwa baraza hilo hadi
kufikia 50 hivi sasa.
Mafunzo
hayo yataendeleo hapo kesho.
No comments:
Post a Comment