Habari za Punde

TPB BENKI YATOA MSAADA VITENDEA KAZI OFISI YA ARDHI MKOA WA TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akipokea msaada wa komputa mbili na printa moja zilizotolewa na Benki ya Posta (TPB)  wenye thamani ya milioni 3.5 kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Benki hiyo Regina Semakafu kwa ajili ya ofisi ya Ardhi Mkoa wa Tanga

BENKI ya Posta imetoa msaada wa vitendea kazi kompyuta mbili na printa moja zenye thamani ya milioni 3.5 kwa ajili ya ofisi ya Ardhi mpya Mkoa wa Tanga ikiwa ni sehemu yao ya kuisaidia jamii katika kutatua changamoto mbalimbali.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,Mkurugenzi wa Fedha wa Benki hiyo Regina Semakafu alisema msaada huo ni wajibu wao kama benki wakiwa wanaihudumia jamii hivyo wakaona umuhimu wa kuisaidia jamii katika kukutana na changamoto mbalimbali.

Alisema kwamba wanaamini hivyo vifaa ambavyo wamevitoa vitasaidia kuwahudumia wananchi na kupunguza changamoto za ofisi mpya ya ardhi mkoa wa Tanga .

“Hivyo tunaamini vifaa tulivyovitoa leo vitasaidia kuwahudumia wananchi na kupunguza changamoto za ofisi mpya ya ardhi mkoa wa Tanga “Alisema Mkurugenzi huyo wa Fedha.

Awali akizungumza mara baada ya kupokea hivyo,Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliishuku Benki hiyo kwa msaada huo ambao wameutoa kwa ajili ya ofisi ya ardhi mkoa huo.

Alisema kwamba kama wanavyofahamu serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt John Magufuli imejipambanua kwenye kufanya maboresho na kutatua changamoto za ardhi katika Taifa letu.

Mkuu huyo wa mkoa alisema ardhi inachangamoto nyingi sana na kwa mkoa huo hivyo anafarijika kuona kwamba ofisi imefunguliwa ikiwa inahitaji mahitaji mengi ikiwemo upatikanaji wa thamani na vifaa kama ambavyo vimekabidhiwa.

“Hivyo niwaambie kwamba mmekuja wakati muafaka kusawaidia na kuwapatia huduma watumishi wetu wa ofisi ya ardhina vifaa hii sio kwamba watavitumia kwa maslahi yao bali ni kwa maslahi ya wananchi wa mkoa wa Tanga “Alisema RC Shigella.

Hata hivyo aliwaishukuru benki hiyo kwa msaada huo huku akieleza kwamba ni matumaini yake kuona vifaa hivyo vinatunza na ili viweze kudumu na kupata thamani.

“Lakini niwaambie wananchi wa mkoa watembelea ofisi ya ardhi wapate hati na waweze kuzitumia kwa ajili ya kukopa na eneo pekee ni benki ya posta lakini wafungue akaunti zao kwenye benki hiyo”Alisema RC Shigella.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.