Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora afanya ziara Mahakama Kuu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman (wakwanza kushoto)  akiingia katika jengo la Mahakama kuu Vuga Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman (katikati) akizungumza na watendaji mbalimbali wa Mahakama kuu ya Zanzibar katika Ofisi ya Jaji Mkuu wa Zanzibar Vuga  wakwanza kushoto ni Jaji Mkuuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kai Bashiru Mbarouk akitoa maelezo kwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman juu ya uchelewaji wa kukamilika kwa jengo jipya la Mahakama kuu ya Zanzibar liliopo Tunguu huko ofisi za  Jaji Mkuu Zanzibar.

Kaimu Katibu Mkuu Katiba na Sheria Daima Mohammed Mkalimoto akitoa ufafanuzi kwa Waziri  wa Nchi Ofisi ya Raisi Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman juu ya ujenzi wa skuli ya sheria huko Ofisi ya Jaji Mkuu Vuga Zanzibar.
Muonekano wa Jengo jipya la Mahakama kuu linaloendelea kujengwa huko Tunguu Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman akitembelea jengo jipya la Mahakama kuu ya Zanzibar lililopo Tunguu kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Mahakama hiyo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman akipata maelekezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kai Bashiru Mbarouk katika Jengo Jipya la mahakama Kuu liliyopo Tunguu Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman akitoa agizo kwa watendaji na wasimamizi  wa Jengo jipya la Mahakama Kuu lililopo Tunguu mara alipofika kwa ajili ya kukagua Jengo hilo .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman akikagua baadhi ya maeneo katika Jengo Jipya la Mahakama kuu linaloendelea kujengwa huko Tunguu Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza ziara yake iliyoanzia Mahakama kuu ya Zanzibar Vuga na kumalizikia jengo jipya la Mahakama kuu Tunguu.

Na Rahima Mohamed   Maelezo      26\11\2020.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman amewataka wafanyakazi wa Mahakama kuwa na ufanisi na mashirikino katika utendaji wa kazi kwani Mahakama ni chombo kikuu cha kutoa haki kwa jamii.

Ameyasema hayo wakati akifanya ziara ya kuitembelea Mahakama kuu ya Zanzibar Vuga pamoja na kuangalia ujenzi wa Mahakama unaoendele Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Amewataka watendaji hao kupambana na rushwa pamoja na kuchukia mambo ambayo yanayoleta athari katika utendaji wa kazi ili kuleta haki kwa waanaostahiki kupata haki hizo.

Hata hivyo Waziri Haroun amesema hakuridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo la Mahakama unaoendelea kwani azma ya Rais wa awamu ya saba Dkt Ali Mohamed Shein kwamba jengo liwe limekamilika ndani ya awamu yake.

Alieleza kuwa jengo hilo liwe limekamilika ifikapo tarehe 31 Disemba mwaka huu lakini kwa hatua iliyofikia hakuna mategemeo ya kumalizika kwa wakati uliopangwa.

“Kwa hatua iliyofikiwa hatuna mategemeo ya kumalizika kwa jengo, sisi kama Serikali hatukuridhishwa na utendaji kazi wa ujenzi wa jengo hilo” alisema Waziri.

Nae Mkandarasi wa jengo hilo Ashish Chopda kutoka kampuni ya Advert Construction amesema kuwa sababu iliyopelekea kuchelewa kukamilika kwa jengo hilo ni pamoja vifaa kutokana na janga la corona.

Aidha amemuhakikishia Waziri huyo ifikapo tarehe 31 Disemba mwaka huu jengo litakuwa limekamilika kwa hatua zote.



 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.