Habari za Punde

KLM Yazindua Safari ya Ndege Yake Kutoka Amsterdam hadi Zanzibar Jana Usiku Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Ndege ya KLM ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikipokelerwa kwa heshima zaote na kurushiwa Maji ikiwa ni ishara ya mapokezi ya Ndege hiyo iliowasili jana usiku ikitokea  Amsterdam na kupokelea na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa..
Ndege ya Shirika la KLM ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume jana usiku ikitikea Amsterdam ilikoaza safari yake hadi Zanzibar ikiwa na Watalii zaidi ya mia moja waliowasili Zanzibar kwa ajili ya Utalii na kutembelea sehemi za Historia ya Zanzibar.
Wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar wakipata picha ya ujiwe wa Ndege ya KLM ilioanza safari zake kati ya Zanzibar na Amsterdam iliowasili jana usiku na kuzinduliwa rasmin Safari yake na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa na Uongozi wa KLM ukingozwa na General Manager Eastern Africa Mr. Arthur Dieffenthaler  wakiipokea Ndege hiyo wakati ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar jana usiku.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe Lela Mohammed Mussa na General Manager Eastern Africa Mr. Athur Dieffenthaler wakikata utepe kuashiri kuzindua Safari ya Ndege ya KLM ilipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Watalii kutoka Amsterdam wakiwasili na Ndege ya KLM katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume jana usiku 


Wziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Lela Mohammed Mussa akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar kwa ujio wa Ndege ya KLM ikizindua safari zake kutoka Amsterdam hadi Zanzibar, uzinduzi huo umefanyika jana usiku wakati wa kuwasili kwa ndege hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar. ikiwa ni safari yake ya kwanza. 

KLM General Manager Eastern Africa Mr. Athur Dieffenthaler akizungumza na Waandishi wa habari ujio wa ndege yao  kutoka moja kwa moja Amsterdam hadi Zanzibar , wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika jana usiku baada ya kuwasili kwa ndege hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.