Habari za Punde

Mafundi, wakufunzi na watawala kuwa makini katika ushughulikiaji na usimamizi wa majengo ya Taasisi

Baadhi ya wakufunzi na watendaji wa utawala kutoka Mamalaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar,wakiwa katika  Mafunzo ya uhifadhi na uimarishaji wa majengo ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar, yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Mwanakwerekwe mjini Unguja.

Mkufunzi wa Mafunzo ya uhifadhi na uimarishaji wa majengo ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar, Muhandisi Salum Ali Juma kutoka Wizara ya Elimu Unguja, akitoa Mafunzo kwa Mafundi, wakufunzi na watendaji wa utawala kutoka Mamalaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar, yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Mwanakwerekwe mjini Unguja.
Mkufunzi wa Mafunzo ya uhifadhi na uimarishaji wa majengo ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhandisi Khamis Rashid Mtara kutoka Wizara ya Elimu Pemba, akitoa Mafunzo kwa Mafundi, wakufunzi na watendaji wa utawala kutoka Mamalaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar, yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Mwanakwerekwe mjini Unguja.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhandisi Idrissa Muslim Hija alipofungua  Mafunzo ya uhifadhi na uimarishaji wa majengo ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar, yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Mwanakwerekwe mjini Unguja.
 


Na Maulid Yussuf, WEMA

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhandisi Idrissa Muslim Hija amewataka mafundi, wakufunzi na watawala kuwa makini katika ushughulikiaji na usimamizi wa majengo ya Taasisi zao ili yaweze kudumu kwa muda mrefu zaidi.
Akizungumza wakati alipofungua Mafunzo ya siku tatu juu ya uhifadhi na uimarishaji wa majengo ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Mwanakwerekwe Mjini Unguja amesema ni vyema kutofanya kazi kwa mazoea ili kuweka ushughulikiaji mzuri wa Majengo ili yawasaidie na wengine.
Dkt Idrissa amesema lengo la mafunzo hayo ni kuelewa namna gani matatizo yanayihitaji kufanyiwa matengenezo baada ya kuharibika na kuweza kuelewa matengenezo yake kwa urahisi kabla ya kuleta athari zaidi.
Aidha amewataka Mafundi na Wakunfunzi hao kuskiliza vizuri mafunzo hayo ili waweze kuyafanyia kazi hasa wakati wa kutumia majengo yao ili lengo liweze kufikiwa la kuleta ufanisi katika kazi.
Dkt Idrissa ameleeza kuwa jengo lolote lilojengwa, ili liendelee kubaki na uzuri wake linahitaji kutunzwa kwa kuhudumiwa, hivyo amewataka kujitahidi kuyatunza vizuri majengo yao ili yabakie katika uhalisia wake.
Hata hivyo amesema Wizara imefanikiwa kuunda Idara itakayoshughulikia majengo yote yaliyo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, na itakuwa na kazi ya kufuatilia kwa karibu majengo yake ya Unguja na Pemba ili panapotokea tatizo liweze kutatuliwa kwa haraka zaidi.
Nae Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vyuo vya Amali Zanzibar Dkt Bakari Ali Silima Amewashukuru Wakufunzi wa mafunzo hayo kwa kuamua kuwapa Elimu watendaji wake juu ya usimamizi ukarabati na utunzaji wa majengo ya Mafunzo ya Amali yakiwemo Daya Mtambwe na Makunduchi.
Amewataka katika mafunzo hayo kujitahidi kufahamu na kuyafanyia kazi ili lengo lililokusudiwa liweze kufikiwa.
Aidha ameleza kuwa usimamizi, utunzaji na ukarabati wa majengo ya Vyuo vya Mafunzo ya Amali unahitaji uendelezwe ili kuhakisha majengo yanabaki katika ubora wake na kudumu kwa Muda mrefu.
Kwa upande wao wakufunzi wa mafunzo hayo Muhandisi Salum Ali Juma kutoka Wizara ya Elimu Unguja na Muhandisi Khamis Rashid Mtara kutoka Wizara ya Elimu Pemba, wamesema kuna umuhimu wa kufanya ukarabati wa Majengo na vifaa ili kuepusha athari kwa watumiaji pamoja na hasara zinazo weza kutokea hapo baadae.
Wamesema wanahitaji kutunza vifaa, samani au majengo kutokana na uwezo wa hali ya nchi ni mdogo ukilinganisha na nchi nyengine, pia kuweka katika uhalisia wake, kuweka uimara wake pamoja na kuepusha athari ambazo zinaweza kutokea.
Mafunzo hayo ya Siku tatu ya utunzaji wa Majengo yamewashirikisha Mafundi, Wakufunzi na watendaji wa Utawala kutoka Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.