Habari za Punde

Serikali haijaridhika na Mfumo wa ukusanyaji wa Mapato viwanja vya ndege

Waziri wa nchi Afisi ya Raisi mipango na Fedha Mheshimiwa Jamal Kassim Ali  akitoa maelezo kwenye moja ya ofisi ya  kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Cha Abeid Aman Karume "A. A. Katika ziara hiyo aliambatana pamoja na waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Rahma Kasim Ali
Baadhi ya wageni waliowasili katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha AAmani Abeid Karume wakiwa katika kukamilisha utaratibu wa kupata Viosa kuwawezesha kuingia nchini
Waziri wa nchi Afisi ya Raisi mipango na Fedha Mheshimiwa Jamal Kassim Ali akitoa maagizo wakati alipofika katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Cha Abeid Aman Karume kwenye ziara yake ya kukagua kiwanja hicho
Waziri wa nchi Afisi ya Raisi mipango na Fedha Mheshimiwa Jamal Kassim Ali  alipofika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Cha Abeid Aman Karume "A. A. Katika ziara hiyo aliambatana pamoja na waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Rahma Kasim Ali


 Waziri wa nchi Afisi ya Raisi mipango na Fedha Mheshimiwa Jamal Kassim Ali alitembelea kiwanja cha ndege cha Kimataifa  Cha Abeid Aman Karume "A. A. Karume International Airport" ili kujionea hali halisi ya Utendaji kazi katika kiwanja hicho. Mhe. Jamal alitembelea sehemu zinazokaguliwa mizigo inayo ingia na kutoka nje ya nchi. Aidha, Mhe. Waziri alikagua sehemu ya kuingia na kutoka kwa abiria kiwanjani hapo. 

Afisa dhamana wa Uhamiaji alimueleza Mhe. Waziri kuwa wanatanua huduma ya vibanda vya kugongea muhuri wa VISA kwa ajili ya kupunguza msongamano kwa abiria wanaosafiri. Aidha, Afisa huyo wa Uhamiaji alimueleza Mhe. Jamal kuwa ndani ya wiki moja vibanda hivyo vitakuwa vimekamilika na vitakuwa 24.

Akizungumza katika ziara ya kuangalia Utendaji wa Bandari na Kiwanja cha ndege cha Abeid Amani Karume akiambatana na Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Rahma Kassim Ali amesema Serikali haijaridhika na Mfumo wa ukusanyaji wa Mapato na kuwataka kuiboresha mifumo hiyo ili kuweza kutoa huduma bora zaidi.

Aidha ameitaka mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar kujiandaa kwa kutoa mafunzo kwa Wafanyakazi wao ili kuweza kufanyakazi kwa ufanisi wakati itakapofika tarehe 31 mwezi ambapo watakabidhiwa kiwanja hicho cha Terminal 3 ili kuweza kuleta ticha kwa Watumiaji na Taifa kwa Ujumla.

 

Nae waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Rahma Kasim Ali amewakumbusha Wafanyabiashara kulipa kodi ili kuiwezesha Serikali kujiendesha kwa kutatua matatizo ya Wananchi ikiwemo Elimu,Afya na Barabara.

Nao baadhi ya Watendaji hao wameahidi kutelkeleza magizo waliopewa licha ya kukabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo udogo wa maeneo ya kufanyia kazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.