BAADHI ya wakufunzi wa ukulima wa mwani Kisiwani
Pemba, wakifuatilia kwa makini mafunzo ya ukulima wa mwani kisasa yaliyotolewa
na taasisi ya REPOA na kufanyika kiwanja cha Makonyo Wawi Chake Chake.(PICHA NA ABDI SUELIMAN, PEMBA)
KATIBU Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya
Viwanda Zanzibar Juma Hassan Reli, akitoa maelezo ya kitaalamu kuhusu mwani
wakati wamafunzo ya ukulima wa mwani kisasa yanayotolewa na taasisi ya REPOA
kwa wakulima 30 watakaoweza kuwafundisha wakulima wenzao vijijini.(PICHA NA ABDI SUELIMAN, PEMBA)
WAZIRI wa Kilimo Umwagiliaji na Mifugo Zanzibar Soud
Nahoda Hassan, akifungua mafunzo kwa wakulima wa mwani 30 juu ya kulima kisasa
wataoweza kuwenda kuwafundisha wakulima wenzao vijijini, yaliyoandaliwa na
taasisi ya REPOA na kufanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SUELIMAN, PEMBA)
MKULIMA wa mwani maarufu Kisiwani Pemba na mbunifu
wa vitu mbali mbali kwa kutumia zao la mwani aliyejulikana kwa jina la Fatma
kutoka Makangale, akitoa neno la shukuran kwa niaba ya wakulima wenzake wa
mwani, katika mafunzo ya ukulima kisasa wa zao hilo yaliyotolewa na taasisi ya
REPOA Tanzania.(PICHA NA ABDI SUELIMAN,
PEMBA)
No comments:
Post a Comment