Na Mwandishi wetu
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ) hakikuridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba kumuachia huru mtuhumiwa aliyembaka mtoto wake wa kumzaa.
TAMWA imepokea taaarifa za Salim Khamis Ali mwenye umri wa miaka (43) mkaazi wa Taifu shehia ya Kinyasini, kisiwani Pemba aliyembaka mtoto wake wa kumzaa huko Pemba ameachiwa huru kwa madai kuwa taarifa za daktari zimeonesha kwamba mtoto huyo ni mzoefu kwa maana ya kuwa ameshatenda tendo la ngono hapo awali.
Tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha polisi Wete tarehe Desemba 6/ 2019 na kufunguliwa jalada namba IR471/2019 ambapo jalada hilo lilieleza kwamba Salim Khamis Ali anatuhumiwa kumbaka mtoto wake wakike aliye chini ya umri wa miaka 13.
No comments:
Post a Comment