Habari za Punde

Tanzania na Hungary zatiliana saini makubaliano ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Kitanzania

 

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Abdallah Possi akisaini makubaliano ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 30 wa Kitanzania Nchini Hungary.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Abdallah Possi akionesha mkataba wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 30 wa Kitanzania mara baada ya kusaini makubaliano hayo.  Balozi wa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na maafisa wa Jamhuri ya Czech mara baada ya kusaini makubaliano ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 30 wa kitanzania nchini Czech.

Tanzania na Hungary zimetiliana saini makubaliano ya ufadhili kwa Wanafunzi zaidi ya 30 wa Kitanzania kwenda kusoma katika vyuo vikuu vya Nchini Hungary katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2021 hadi 2023.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Ujerumani anayeiwakilisha pia Hungury Dkt. Abdalla Possi amesema makubaliano hayo yanatoa fursa kwa Wanafunzi wa Tanzania kupata elimu katika Vyuo vya Hungary kwa masomo ya shahada ya kwanza,shahada ya Uzamili na shahada ya uzamivu katika maeneo mbalimbali ya kitaaluma.

Ameongeza kuwa makubaliano hayo ni kielelezo kingine cha uhusiano mzuri uliopo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Hungury na kwamba nafasi hizo zitaendelea kuongezeka kutokana na Serikali ya Hungary kufurahishwa na muitikio wa Watanzania wanaoomba nafasi hizo za masomo.

Katika tukio jingine Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ujerumani umefungua rasmi ofisi ya muwakilishi wa heshima wa Tanzania iliyoko katika mji wa Bruno katika nchi ya Jamhuri ya Czech.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemuidhnisha Bw. Roman Grolig kuwa mwakilishi wa heshima wa Tanzania katika Jamhuri ya Czech ambapo mji wa Bruno ni mji wa kimkakati ambapo kila mwaka mamlaka za mji huo huandaa miongoni mwa mambo mengine maonesho makubwa ya biashara na utaliibarani Ulaya.

Mji wa Bruno pia ni makao makuu ya Baraza la biashara la Czech – Tanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.