Habari za Punde

Timu ya Taifa ya Uganda U-20 Yaibuka Bingwa wa Michuano Hiyo Kwa Kuifunga Tanzania U-20 Kwa Mabao 4-1

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Disemba 2, 2020 amehudhuria fainali michuano ya CECAFA U-20  iliyofanyika katika kituo cha michezo cha Black Rhino kilichopo Karatu, Mkoani Arusha.

Katika mchezo huo ambao Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa mgeni rasmi, ulizikutanisha timu za Tanzania na Uganda. 

Katika mchezo huo timu ya taifa ya Uganda chini ya miaka 20 iliifunga timu ya Taifa ya Tanzania ambaye ndiye alikuwa bingwa mtetezi magoli Manne (4) kwa Moja (1).

Bingwa wa michuano hiyo ni Timu ya Taifa ya Uganda U-20, mshindi wa pili ni timu ya taifa ya Tanzania U-20 na mshindi wa tatu ni Timu ya taifa ya Sudani Kusini U-20.


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.