Habari za Punde

Hafla ya kuwaaga wastaafu Idara ya Habari Maelezo

Mfanyakazi wa Kitengo cha mawasiliano Ikulu Zanzibar Mwatima Rashid Issa akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wafanyakazi wa Ikulu Zanzibar katika hafla ya kumuaga Mfanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo kitengo cha vipaza sauti katika ukumbi wa sanaa Rahaleo Zanzibar.

Baadhi ya wafanyakazi idara ya Habari Maelezo Zanzibar wakifuatilia hafla ya kuagwa kwa Mfanyakazi mwenzao Omar  Sleiman Othman kutoka kitengo cha vipaza sauti huko Ukumbi wa sanaa Rhaleo Mjini Zanzibar.
Kaimu Mkurugrenzi Idara ya Habari Maelezo Omar Saidi akimkabidhi cheti cha ustaafu aliekuwa mfanyakazi wa Idara ya habari Maelezo kitengo cha Vipaza sauti Omar Sleiman Othman huko Ukumbi wa sanaa Rahaleo Mjini Unguja.

Aliekuwa mfanyakazi wa Idara ya habari Maelezo kitengo cha Vipaza sauti Omar Sleiman Othman akitoa shukurani kwa wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar katika hafla ya kuagwa iliyofanyika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Zanzibar.

PICHA NA MARYAM KIDIKO MAELEZO/ ZANZIBAR.

Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 03/-1/2021.

Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya Habari Maelezo Omar Said Ameir amewataka wafanyakazi wa Idara hiyo, kuwa wabunifu na wawajibikaji katika kutekeleza majukumu yao.


Aliyasema hayo katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo wakati wa hafla ya kumuaga aliekuwa fundi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Omar Suleiman Othman (Omar Mabomba) ambae amestaafu kwa mujibu wa sheria.   


Alisema Idara ya Habari Maelezo ni msemaji wa shughuli za Serikali, kuelezea mafanikio ya miradi inayotekelezwa na changamoto inayoikabili miradi hiyo.


Aliwashauri Wafanyakazi wa Idara hiyo kubadilika kwa kuongeza nidhamu katika utendaji wao wa kazi kwani siri ya mafanikio ya kazi ni nidhamu.


Kaimu Mkurugenzi aliwakumbusha wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo kwamba maafisa wote wa habari wa Taasisi za Serikali wapo chini yao hivyo wanawajibu wa kuwapa ushirikiano ili kufanikisha kazi zao.


Nae mstaafu Omar Sleiman Mabomba aliwashauri wafanyakazi wa Idara hiyo kujituma zaidi na kupenda kazi pamoja na kufuata sheria na kanuni za kazi .


“Siri kubwa ya mafanikio katika kazi ni kutunza nidhamu kwa wakubwa na wadogo, kudumisha upendo mashirikiano katika kazi,”alisisitiza Fundi Mkuu Mstaafu.


Awali Afisa Habari wa Kitengo cha Mawasiliano  Ikulu Mwatima Rashid Issa kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ametoa pongezi kwa mstaafu Omar Suleiman kutokana na uwadilifu wake na kuipenda kazi yake wakati wote alipokuwa kazini.


Amemshukuru kwa juhudi kubwa aliyoonyesha wakati wa utumishi wake wa kazi na kuwa mfano kwa wafanyakazi wenzake na aliwataka kufuata nyayo za mstaafu huyo.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.