Habari za Punde

NAIBU WAZIRI UMMY ATEMBELEA WAENDESHA BAJAJI WENYE ULEMAVU FERRY, JIJINI DAR ES SALAAM

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga kushoto akimsikiliza mmoja wa wakilishi wa Umoja wa Waendesha Bajaji wenye Ulemavu Bw. Juma Bilali (katikati) alipowatembelea kwa lengo la kusikiliza kero zinazowakabili.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (kulia) akizungumza na Umoja wa Waendesha Bajaji wenye Ulemavu alipowatembelea katika eneo la Ferry, Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kero zao. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka, Mhandisi Ronald Rwakatare. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kushoto aliyesimama) akimsikiliza Ndg. Mwinyi Singa (aliyekaa wenye ulemavu) alipokuwa akiwasilisha changamoto wanazokabiliana nazo katika utendaji wao wa shughuli ya uendeshaji bajaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka, Mhandisi Ronald Rwakatare (kulia) wakati wa ziara yake hiyo, Jijini Dar es Salaam.
Dereva wa Bajaji. Bi. Evodia Nchimbi akieleza baadhi ya kero zinazowakabili kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (hayupo pichani) wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Ndg. Jumanne Shauri akileza jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga (hayupo pichani) kuhusu fursa za mikopo inayotolewa na halmashauri.
Baadhi ya Waendesha Bajaji wenye Ulemavu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya alipotembelea umoja huo wa Waendesha Bajaji wenye Ulemavu kutembelea kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuzitatua.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.