Habari za Punde

RC Mjini Magharibi alivalia njuga sakata la magari mabovu yaliyonunuliwa kwa ajili ya Manispaa ya Mjini

Sehemu ya Magari yaliyonunuliwa kwa ajili ya Manispaa lakini hayakuwa na viwango na mengine ni mabovu
Sehemu ya Magari yaliyonunuliwa chini ya mradi wa ZUSP kwa ajili ya Manispaa lakni hayakuwa na viwango na mengine ni mabovu
MKUU wa mkoa Mjini Magharibi Mhe Idrissa Kitwana Mustafa  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la magari 

 Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka akizungumzxa na wanahabri juu ya sakata hili na kuahidi ndani ya masaa 48 watawaita tena waandishi wa habari kuwajuza mtu aliyeyanunua magari yasiyo na viwango na kuitia hasara serikali

MKOA MJINI MAGHARIBI                                                                


MKUU wa mkoa Mjini Magharibi Mhe Idrissa Kitwana Mustafa ameugiza uongozi wa wilaya ya Mjini kushirikiana na baraza la manispaa hiyo kumtafuta msambazaji na muingizaji wa gari za manispaa zilizoletwa kwa ajili ya shughuli za usafi.


Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo kufuatia ziara yake shehia Shaurimoyo Santana katika eneo la manispaa ya mjini kuangalia mgagari 6 kati 17 ya kufanyia usafi kwa manispaa ya mjini zilizotolewa katika mradi wa zusp ambazo zinasadikiwa kukosa ubora kulingana na gharama za fedha zilizonunuliwa.


Amesema gari hizo zimewekwa katika eneo hilo zaidi ya miezi sita hatua ambayo inaashiria kuwepo kwa ukiukwaji wa sheria na matumizi mazuri ya mali za serikali na ubadhirifu wa mali umma.


“Nataka mkuu wa wilaya na kaimu mkurugenzi hakikisheni mnachukua hatua za haraka mnampata aloingiza na aliezitoa bandarini gari hizi ili atueleze ilikuwaje bodi ya inasomeka ISUZU lakini injini inasomekia jina jengine,” alisema mkuu wa Mkoa.


Aidha Mhe Kitwana amesema serikali ya mkoa huo haiwezi kulivumilia suala hilo na itahakikisha inapambana kwa nguvu zote katika masuala ya uzembe,rushwa na ubadhilifu wa mali za umma ili kuona fedha za serikali zinazotumika zinaleta tija kwa jamii.


Mapema naibu Kamishna wa TRA Zanzibar Mcha Haji Mcha amesema gari hizo sita wamekabidhi na mamlaka ya Bandari kisheria ili kuzipiga mnada au kuzitowa kwa taasisi nyengine za serikali kwa vile manispaa ya mjini imezikataa kwa madai hazina ubora.


“Sisi kama TRA tumekabidhiwa gari hizi kupitia mamlaka ya bandari tuyapige mnada kwa vile manispaa imezikata kulingana na ubora wake na kwa mujibu wa sheria na mamlaka tuliyonayo tunaweza kuyauza au kuyagawa kwa taasisi nyengine ya serikali na sasa tupo katika mundelezo wa taratibu hizo,” alisema naibu kamishna TRA.


Kaimu mkurugenzi manispaa ya Mjini Sleimani Mohammed Rashid na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka wamesema watahakikisha wanampata mtu aliengia mkataba na kuleta gari hizo si zaidi ya masaa 24 na kwamba baada ya kukamilisha taratibu za kisheria watahakikisha hawatoi kazi nyengine kwa msambazaji huyo kutoka kwa manispaa hiyo kwa hasara kubwa waloiyoitia serikali.


Wamesema kufuatia kuingiza gari zisizo na ubora na kuitia hasara kubwa manispaa kwani imekuwa ikifanya kazi za usafi katika mazingira magumu kwa kipindi kikubwa chini ya kiwango kutokana na uhaba wa vifaa viliopo na mahitaji waliyonayo.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.