Habari za Punde

Yanga yalazimishwa sare na Jamhuri. Hakuna Mbabe Mapinduzi Cup


 Mshambuliaji wa Timu ya yanga Waziri Juniro akimtoka Beki wa Jamhuri wakati timu hizi zilipokutana jana usiku na kutoka sare bila ya kufungana


Na mwandishi wetu

KLABU ya soka ya Yanga imeshindwa kutamba mbele ya Jamhuri kwa kulazimishwa sare isiyokuwa na magoli katika mchezo wa mashindano ya kombe la Mapinduzi uliochezwa usiku wa kuamkia jana.

Mchezo huo ambao wengi wa mashabiki waliokuwepo hapo hawakuweza kuamini na kilichotokea ulichezwa katika uwanja wa Amaan mjini Unguja.

Katika mchezo huo ambao ni wa ufunguzi mgeni rasmi alikuwa ni Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman, ambae aliungana na wadau wa mchezo huo waliofika uwanjani hapo.

Miamba hiyo ambayo ilikuwa ikishambuliana kwa zamu ilienda mapumziko wakiwa hakuna ambae alieouna mlango wa mwenziwe.

Kipindi cha pili kilianza na mashambulizi kama kawaida yakaendelea, huku Yanga ambayo ilijaribu kuliandama sana lango la wapinzani wao wakajikuta mashuti yao yote yakiishia miguuni kwa walinzi wa Jamhuri.

Jamhuri ambayo ilitoa mchezaji bora wa mchezo huo Ali Juma na kuzawadiwa pesa taslimu na Shirika la Bima la Taifa Tanzania (NIC), walionesha kiwango cha hali ya juu ambacho hakuna ambae aliweza kufikiria matokeo yake.

Timu hizo zilijaribu kufanya mabadiliko ya mara kwamba lakini hadi mwamuzi wa mchezo huo Nassir Msomali anapuliza kipenga cha kumalizia dakika 45 za pili matokeo yakabakia ni 0-0.

Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu tisa inatarajiwa leo kuendelea tena kwa kuchezwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Yanga na Mlandege ambao utachezwa saa 2:00 za usiku

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.