Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi Amejumuika na Wananchi wa Zanzibar Katika Kisomo cha Hitma na Dua Kumuombea Marehemu Seif Sharif Hamad Viwanja vya Maisara Jijini Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Maisara Suleiman kuhidhuria kisomo cha Hitma na Dua kumuombea aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, kilichofanyika leo jioni katika viwanja hivyo akiongozana na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume. 
Rais wa Zanzibar nba Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua kabla ya kuaza kwa kisomo cha Hitma na Dua ya kumuombea aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Marehemu Seif Sharif Hamad, iliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman leo jioni baada ya Sala ya Alasir na (kulia kwa Rais) wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali.
Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Sita Alhajj Dk. Amani Karume na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uwekezaji na Uchumi Mhe Mudrik Soraga wakiitikia dua kabla ya kuaza kwa kisomo cha hitma na dua ya kumuombea aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Marehemu Seif Sharif Hamad, iliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.