Habari za Punde

Kuapishwa Kwa Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Walioteuliwa Hivi Karibuni.

MAJAJI Wateule wa Mahakama Kuu Zanzibar wa kwanza Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim, Mhe. Haji Omar Haji na Mwenyekiti Mteule wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Bi. Khadija Shamte Mzee, wakiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar wakisubiri kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi hafla hiyo imefanyika leo Ikulu.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisaini hati ya Kiapo ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim, baada ya kumuapisha leo 8-2-2021 Ikulu Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Haji Omar Haji kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Bi. Khadija Shamte Mzee kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Hati ya Kiapo Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Bi.Khadija Shamte Mzee baada ya kumaliza kula kiapo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 8-2-2021
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi wakifuatilia kuapishwa kwa Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
MAJAJI wa Mahakama Kuu Zanzibar, wakifuatilia kuapishwa kwa Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.