Habari za Punde

Wakamatwa kwa utapeli mtandaoni mjini Telangana

Watu watatu akiwemo raia wa China wamekamatwa na polisi wa jijini la Telangana baada ya kulalamikiwa na mkazi wa mji huo aliyedai kusumbuliwa na kampuni za programu za mkopo mtandaoni zilizomtaka kulipa kiwango cha juu cha riba.

Polisi katika mji huo wamesema wamekamata kituo cha kupiga simu cha Pune kinachodaiwa kutumika kuwasumbua wakopaji wa kampuni za programu za mtandaoni ili kurejesha mikopo na kuwakamata watu hao.

Watu hao waliokamatwa Ijumaa iliyopita wanadaiwa kulazimisha kupata fedha wakitumia  programu 11 za mkopo wa papo kwa papo walizozitengeneza.

Ukandamizaji dhidi ya kampuni za kukopesha pesa papo hapo umezinduliwa baada ya matukio matatu ya kujiua pamoja na lile ya mhandisi wa programu ikiwa ni kwa sababu ya unyanyasaji wa kampuni hizo ziliripotiwa huko Telangana takribani mwezi mmoja uliopita.

“Waliokamatwa hivi karibuni ni mkurugenzi wa kituo cha kupigia simu huko Pune, mkewe ambaye ni raia wa China anayesaidia kuendesha shughuli za kampuni pamoja na meneja wa rasilimali watu,” amesema kamishna wa Polisi wa Rachakonda, Mahesh Bhagwat.

Polisi wamesema kwa sasa  takribani wafanyikazi 650 waliokuwa wakifanya kazi katika kituo cha kupiga simu, wameagizwa kutumia namba zao binafsi za simu kuwapigia wakopaji, jamaa zao, marafiki na kusisitiza ulipaji pamoja na riba.

Kwa mujibu wa polisi, kampuni zinazotoa mikopo kupitia programu za mkopo wa papo kwa papo zilitoa mikopo kwa watu binafsi na kulipia riba kubwa na ushughulikiaji wa mashtaka kati ya wengine na kutumia dhuluma, kusumbua, na kutishia waliokiuka kupitia vituo vya kupiga simu.

“Wanawahadaa wakopaji kwa kutuma taarifa bandia za kisheria kwa jamaa zao na wanafamilia. Kesi zimesajiliwa katika vituo vya polisi katika jimbo hilo kwa mujibu wa malalamiko kadhaa kwamba kampuni hizi zinadaiwa kupata data nyeti kama mawasiliano, picha kutoka kwa simu za mkononi za wateja na kuzitumia kukashifu au kushawishi kupata malipo ya mkopo,”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.