Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Atoa Mkono wa Pole Kwa Familia ya Mchezaji Maarufu Zanzibar Salum Mkweche Aliyefariki Hivi Karibuni.

Bwana Ali Salum, Mtoto wa Marehemu Veterani wa Michezo Nchini Mzee Salum Mkweche kwa niaba ya wanafailia akiishukuru Serikali na Viongozi wake kwa jinsi walivyoungana na familia hiyo katika msiba wa Mzazi wao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman na Wanafamilia hao kwa pamoja wakimuombea Dua ya safari ya salama Veterani wa Michezo Nchini Marehemu Salum Mkweche alipofika nyumbani kwao Kokoni Wilaya ya Mjini kutowac mkono wa Pole kwa Wnafamilia.Picha na – OMPR – ZNZ.

Na.Othman Khamis.OMPR. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali imeguswa na kufikia uamuzi wa kuungana na wanafamilia pamoja na Wanamichezo wote kwenye msiba wa Viterani wa Michezo Nchini Mzee Salum Mkweche.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo alipofika nyumbani kwa mwanamichezo huyo Kokoni Mjini Zanzibar, kwa ajili ya kutoa pole kwa familia ya marehemu huyo, kwa kuondokewa na mzee wao.

Mheshimiwa Hemed amesema kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar anawapa pole famillia hiyo, na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hichi cha Msiba na kusema kuwa serikali inatambua mchango wa Veteran huyo na imepokea kwa masikitiko taarifa ya msibawake.

Mheshimiwa Hemed ameendelea kueleza kuwa licha ya uhodari wake katika michezo marehemu Mzee Mkweche alikuwa na ufasaha wa kuzungumza, ulioambatana na ucheshi kwa wanamichezo wenzake na hata  jamii iliyomzunguuka.

Akitoa salamu za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dr Hussein Ali Mwinyi, Mheshimiwa Hemed amesema  Dr Mwinyi anawapa pole watoto wa marehemu na wanafamilia hao, na kuwa anatambua mchango wa Mwanamichezo huyo wa zamani nchini, na kuwa yupo pamoja na Familia hiyo katika kipindi hichi kigumu.

Kwa upande wao Wanafamilia hao wakiwasilishwa na Mmoja wa  Mtoto wa Marehemu Bwana Nassor Salum Mkweche amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa, Marehemu alikuwa ni Mwanamichezo aliyesifika kwa kipaji cha kipekee ambacho ndicho kilichompatia hadhi na kuwa maarufu katika michezo.

Aidha amesema Marehemu Mzee Mkweche aliishi vizuri na watoto wake kwa ukaribu zaidi, hali ambayo iliwajenga watoto hao kuwa na Umoja na Mashirikiano zaidi, licha ya kuwalea katika hali duni ya kiuchumi.

Akielezea sababu ya kifo chake amesema Marehemu licha ya utu uzima wake, Afya yake ilibadilika ndani ya kipindi cha wiki mbili hadi alipoonja mauti kama inavyoilazimu nafsi yoyote ya kiumbe.

Marehemu Viterani wa Michezo Nchini Mzee Salum Mkweche amezikwa Jumapili ya tarehe 31 Januari katika makaburi ya Mwanakwerekwe.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Aamin.

1 comment:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.