Habari za Punde

Makamu wa Rais Mhe Samia mgeni rasmi maadhimisho ya kutimia miaka 44 ya Chama cha Mapinduzi CCM

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam alipowasili katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwabwepande kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa Hadhara katika Maadhimisho ya kutimia miaka 44 ya Chama cha Mapinduzi CCM leo Febuari 06,2021.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Tuzo aliyokabidhiwa na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kinondoni kwa kutambua mchango wake mkubwa alioutoa kwa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam, wakati wa Maadhimisho ya kutimia miaka 44 ya Chama cha Mapinduzi CCM yaliyofanyika leo Febuari 06,2021 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwabwepande Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipanda Mti aina ya Mfenesi mbele ya Jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Mwabwepande Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam baada ya kuweka Jiwe la Msingi Ofisi hiyo leo Febuari 06,2021 katika Maadhimisho ya kutimia miaka 44 ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka jiwe la msingi Ujenzi wa Jengo la Hospitali ya Kisasa ya Wilaya ya Kinondoni katika eneo la Mwabwepande Jijini Dar es salaam leo Febuari 06,2021. kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Mama Kate Kamba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.