Habari za Punde

Mkutano wa Wadau wa Oporesheni ya Kupambana na Dawa za Kulevya Kisiwani Pemba.

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud, akifungua mkutano wa wadau wa Operesheni na udhibiti wa dawa za kulevya Pemba, ulioandaliwa na Tume ya Kitaifa ya kuratibu na udhibiti wa dawa za kulevya, kutoka Ofisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais na kufanyika mjini Chake Chake
AFISA Mdhamini ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Ahmed Abubakar Mohamed, akizungumza na wadau wa Operesheni na udhibiti wa dawa za kulevya Kisiwani Pemba, mkutano uliofanyika ofisi za DPP Madungu Chake Chake.
AFISA Sheria kutoka Tume ya Kitaifa ya kuratibu na udhibiti wa dawa za kulevya, kutoka Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais, Daudi Juma Suleiman, akiwasilisha mada ya kwanza katika mkutano wa wadau wa Operesheni na udhibiti wa dawa za kulevya uliofanyika mjini Chake Chake.

AFISA kutoka Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba Issa Abass Mohamed, akiwasilisha taarifa ya dawa za kulevya kwa kipindi cha 2020, wakati wa mkutano wa wadau wa Operesheni na Udhibiti wa dara za Kulevya Pemba, mkutano uliofanyika mjini Chake Chake.
WADAU wa Operesheni na Udhibiti wa Dawa za Kulevya Kisiwani Pemba, wakiwa katika mkutano wa uwasilishaji wa taarifa za matukio ya Dawa za kulevya kwa mwaka 2020, mkutano uliowashirikisha ZAECA, KM KM, POLISI, DPP na watendaji kutoka Tume ya Kitaifa ya Kuratib na udhibiti wa dawa za kulevya Pemba.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.