Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Wawi akabidhi mifuko 30 ya Saruji kwa tawi la CCM Mkoreshoni kisiwani Pemba

MWAKILISHI wa Jimbo la Wawi Kisiwani Pemba Bakar Hamad Bakar kulia akimkabidhi mifuko 30 ya saruji, Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa Mikoa Miwili ya Pemba, Makongoro Julius Nyerere kwa ajili ya upigaji wapalasta ndani na nje tawi la CCM Mkoroshoni, ikiwa ni shamra shamra za kutimiza miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MJUMBE wa kamati kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa Mikoa Miwili ya Pemba, Makongoro Julius Nyerere akizungumza na wanachama wa CCM Tawi la Mkoroshoni, kabla ya kukabidhi mifuko 30 ya saruji na kupigisha harambee ya ujenzi huo ambapo shilingiu 1595000/= zilikusanywa na fedha taslimu  shilingi laki 835000/= ahadi shilingi laki 760000/=.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MJUMBE wa kamati kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa Mikoa Miwili ya Pemba, Makongoro Julius Nyerere katikati, akipiga makofi na viongozi wengine wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba, mara baada ya kuwasili katika tawi la CCM Mkoroshoni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.