Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi amtengua Mkurugenzi wa ZBC na kuivunja Bodi ya ZBC

 Na Ali Issa Maelezo Zanzibar 5/2/2021

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussen Ali Mwinyi amemtengua Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC pamoja na kuvunja bodi ya ZBC na kuchaguliwa mwenyekiti mpya wa bodi ya ZBC ndugu Ali Mohamed Uki.

Akitoa Taarifa kwa vyombo vya Habari huko Ofini kwake Migombani Waziri wa Habari,vijana  Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita amesema hatua ya kutenguliwa Mkurugenzi na kuchaguliwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya ZBC ni kutokana na Uchunguzi wa kamati ilioundwa na wizara ya habari  disemba 17 2020 kulichunguza shirika la Utangazaji ZBC na ZMUX kutokana na mwenendo wake usio ridhisha na  kutokuwa makini.

Amesema kamati imefanya kazi zake vizuri kama ilivyo agizwa na tayari Ripoti ya matokeo ya uchunguzi yameshapelekwa kwa Mh.Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT. Hussen Ali Mwinyi kwa ukamilifu wa kazi hiyo.

Amesema katika uchunguzi wa kamati hiyo kulichunguza shirika la utangazaji la ZBC na ZMUX kilicho bainika ni kwamba Mikataba mikubwa iliofungwa haikuonesha uhalisi wake,jambo ambalo ni uzembe mkubwa ulio fanywa.

Aidha alisema kuwa mfumo wa uajiri wa ZBC ni mbovu ambao haukufuata mfumo wa utumishi kwa asilimia 85 na uko chini ya kiwango ambao waajiriwa wengi wamekosa sifa ya kufanya kazi.

Hata hivyo aliongeza kusema kuwa imegundulikana kuwa majengo ya ZBC yamechakaa vibaya hayaendani na hadhi ya shirika la utangazaji kituambacho ni kupuuza dhana ya habari na mawasiliano.

Pia waziri huyo aliongeza kwa kusema shirika hilo halina muongozo unao fuatwa na wafanya kazi,hakuna uwajibikaji,nidhamu,kilammoja anafanya analotaka yeye.

Pamoja na hayo pia alisema kuwa uchunguzi ulibaini kunamalimbikizo makubwa ya madeni,shirika linashindwa kujiendesha,kunaupotevu mkubwa wa mapato na shirika halikufanyiwa ukaguzi wa Fedha kwa muda wa miaka miwili,pia na kuwepo changamoto kubwa ya kutotuza kumbukumbu za shirika 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.