Habari za Punde

Wanasheria Wanawake Zanziba ZAFELA Watakiwa Kutumia Elimu Yao Kupinga Vita Vitendo vya Udhalilishaji


Mkururgenzi wa Jumuiya hiyo Bi Jamila Mahmoud Juma Kushoto akielezea mafanikio ya Jumuiya yao ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) jinsi inavyoendelea   kutoa elimu kwa jamii hasa vijijini. wa Jumuiya hiyo Bi Jamila Mahmoud Juma Kushoto akielezea mafanikio ya Jumuiya yao ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) jinsi inavyoendelea   kutoa elimu kwa jamii hasa vijijini.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed akizungumza na Viongozi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) walivyofika Ofisini kwake Vuga kujitambulisha.Picha na – OMPR – ZNZ.

Na.Othman Khamis .OMPR.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amewataka Wanasheria kutumia Elimu waliyonayo katika kuendeleza vita dhidi ya kupinga vitendo vya udhalilishaji, sambamba na kuelimisha ubaya wa rushwa.

Mheshimiwa Hemed ameyasema hayo alipokutana kwa mazungumzo na Viongozi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) walivyofika Ofisini kwake Vuga kujitambulisha.

Amesema umefika wakati kila mmoja kwa mujibu wa nafasi na elimu aliyonayo kujikita zaidi katika kuungana na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane, kwa kuendeleza kupiga vita suala la Udhalilishaji linalowakumba zaii Watoto na Akinamama.

Mh. Hemed alibainisha kwamba katika mapambano hayo Serikali tayari imeshaanza utaratibu wa kuzipitia Sheria zote zinazohusinana na vitendo vya udhalilishaji, ili iwe rahisi katika uendeshaji wa kesi za aina hiyo, na kuisihi jamii kuwacha tabia ya umuhali katika kutoa ushahidi kwenye kesi.

Ameipongeza Jumuiya ya Zafela kwa kazi wanazoendelea kufanya hasa  kwa kuwaelemisha kina mama, kuhusu uelewa wa sheria ili waweze kujua haki stahiki zao, na kuongeza kuwa kina mama wana nafasi kubwa ya kushawishi jamii kuondokana na tabia hiyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka Wanansheria hao kutokata tamaa na kutovunjika moyo, katika kazi wanazozifanya na badala yake waungane na kasi ya Serikali yenye lengo la kutaka kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Kwa upande wake Mkururgenzi wa Jumuiya hiyo Bi Jamila Mahmoud Juma alisema Jumuiya hiyo imefanikiwa kutoa elimu kwa jamii hasa vijijini na kueleza kuwa wamekutana na changamoto mbali mbali ikiwemo uelewa mdogo wa jamii juu ya suala la udhalilishaji na hata elimu ya rushwa.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar Bi Safia Hija amesema jumuiya yao imeanzishwa mnapo mwaka 2003 na kupatiwa usajili 2005, ikiwa na lengo la kutoa huduma za kisheria kwa Wanawake na Watoto.

Bibi Safia alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba  Taasisi yao ya Kisheria imepata mafanikio makubwa kwa kuwasaidia akina mama Mahakamani ili kupata haki zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.