Habari za Punde

IGP Sirro Afungua Mkutano wa Wakurugenzi wa Upelelezi Kwa Njia ya Video Conference.

 

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika (EAPCCO) ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Shirikisho hilo kutumia fursa ya mazungumzo kwa kujadiliana masuala ya ugaidi, ukatili wa kijinsia pamoja na masuala ya haki za binadamu.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akifungua mkutano wa Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika mkutano ambao umefanyika kwa njia ya mtandao video conference na kuhusisha nchi wanachama 14 wa EAPCCO kwa lengo la kufanya nchi hizo wanachama kuendelea kuwa salama.

Kwa upande wa changamoto IGP Sirro amesema, zipo changamoto zilizopatiwa ufumbuzi na kwamba bado shirikisho hilo linaendelea na jitihada mbalimbali ikiwemo operesheni za pamoja na mafunzo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.