Habari za Punde

Ni muhimu kuimarisha usafi wa miji ya Zanzibar : Mhe Hemed

Mtaalamu kutoka Land Consutancy Limited Dk. Aleshiwa Clara akiwasilisha akielezea juu ya muonekano wa ramani ya mkoa wa mjini Magharibi itakayojumisha ujenzi wa madaraja baharini yakiuunganisha mji mkongwe wa Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwasisitiza na watendaji wa taasisi za serikali juu ya umuhimu wa kuimarisha usafi wa mji katika kikao maalum cha uwalishilishaji wa maelezo ya mradi uliondaliwa na Kampuni ya VIGOR kwa kushirikiana kwa kushirikana na Land Consultance Limited.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwasisitiza na watendaji wa taasisi za serikali juu ya umuhimu wa kuimarisha usafi wa mji katika kikao maalum cha uwalishilishaji wa maelezo ya mradi uliondaliwa na Kampuni ya VIGOR kwa kushirikiana kwa kushirikana na Land Consultance Limited.

Na Kassim Abdi, OMPR

Mamlaka zinazosimamia miji zimetakiwa kuendeleza kazi ya usimamizi wa suala la usafi wa mji ili kuungana na kauli ya Mhe. Rais katika  kupendezesha haiba ya Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla  alitoa kauli hiyo katika uwasilishaji wa maelezo ya mradi wa kusimamia usafi wa mji kupitia wazo lililoandaliwa na Kampuni ya VIGOR na kuwashirikisha washauri elekezi kutoka Land Consultancy Limited.

Mhe. Hemed alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuimarisha usafi wa miji ya Zanzibar kutokana na mchango wake wa kuinua umchumi wa nchi kupitia sekta ya utalii.

Alieleza kuwa kitendo cha kuweka safi mazingira ya miji yetu kinasaidia kuvutia watalii kutembelea Zanzibar katika maeneo mbali mbali ikiwemo sehemu za kihistoria na kupelekea nchi kupata fedha za kigeni.

Kutokana na mchango huo kupitia usafi wa miji Mhe. Hemed aliwashauri viongozi na wasimamizi wa Miji, manispaa pamoja na halmashauri kuckua jitihada za maksudi katika kuhakikisha maeneo yanakuwa safi ikiwa pamoja na kuweka mpangalio mzuri wa ramani zake.

Akizungumzia juu ya wazo hilo Makamu wa Pili wa Rais alipongeza kampuni ya VIGOR kwa kushirikiana na Land Consultancy Limited kwa kuja na wazo zuri kwa wakati muafaka na amewahidi serikali itatoa ushirikiano stahiki kwa kuwapa kipaumbele.

“Serikali inatoa kipaumbele kwa wazawa katika kuimarisha maendeleo ya nchi, hivyo nawahidi ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha mpango wa kuimarisha Usafi wa mji” Alisema Mhe. Hemed

Katika kuhakikisha miradi inayoanzishwa inafanikiwa Mhe. Hemed alipendekeza kuwepo kwa ushirikishwaji wa wataalamu kutoka sekta zote kuanzia mwanzo wa mradi ili kupata mawazo yatakayosaidia kukamilika kwake bila ya kutokea athari za kimazingira.

Nae Mwenyekiti wa Kampuni ya VIGOR Mhe. Slum Taufiq Turky alimuleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa sekta binafsi zimeamua kuja na mipango ya kuisaidia nchi kutokana na maelekezo yaliotolewa na Mhe. Rais kwa kuzitaka sekta binafasi kushirikiana na serikali.

Alisema maelezo hayo ya mradi yaliowasilishwa endapo yatafanikiwa kutekelezwa yatajibu changamoto nyingi zinazoikabili miji yetu katika eneo la la usafi pamoja na masuala ya usafiri.

Akiwasilisha ramani ya mji utakavyokuwa kwa mkoa wa mjini Magharibi Dk. Aleshiwa Clara alileza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kufanya mji wa Zanzibar kuwa kitovu cha utalii kwa kujenga madaraja ya kuvutia  yatakayopita baharini na kuunganisha na mji mkongwe mji wa Zanzibar.

Wakiwasilisha mada ya udhibiti wa tanga pamoja na mfumo wa usafiri Injinia Jonas Gerevas Balengayabo na Injinia Allbert BModest Mwauzi walisema taka zinaweza kudhibiwa kwa kuandaa mfumo maalum wa kuzitumia taka hizo katika uzalishaji wa nishati ya umeme pamoja utengenezaji wa Mbolea.

Walisema zipo nchi zimefanikiwa  kutumia taka katika uzalishaji wa umeme unaotokana na Gesi jambo ambalo limetoa tija kwa kustawisha maisha ya jamii baada ya kufunga vifaa na mitambo maalum ya kuzalishia umeme.

“ Zanzibar inaweza kukopia utaalamu kutoka sehemu nyengine juu ya matumizi sahihi ya taka kwa ajili ya kuzalishia nishati mbdala”

Wakichangia mada zilizowasilishwa washiriki wa kikao hicho walisema taasisi hiyo inapaswa kufanya utafiti Zaidi juu ya maelezo ya mradi huo ili uweze kutoa tija kwa jamii na kuimarisha hali zao za kimaisha.

Walieleza kuwa miradi itakayoekezwa Zanzibar lazima mwanzo wa utekelezaji wake inufashie serikali pamoja na wananchi wakitolea mfano suala la upatikanaji wa ajira.

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.