Habari za Punde

Wataalamu wa Tiba ya Kisuna Watakiwa Kujisajili

Katibu wa Mufti Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume akizungumza na Wadau wa Tiba za kisuna (hawapo pichani) ofisini kwake Mazizini kuhusu utaratibu mpya  wa kujisajili katika ofisi hiyo ili waweze kutambulika rasmi.

Wadau wa Tiba za ksiuna na miti shamba wakimsikiliza katibu wa Mufti  (hayupo pichani) kuhusu utaratibu mpya  wa kufuatwa kwa wadau wa fani hiyo ofisi kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar

Na Mwashungi Tahir    Maelezo Zanzibar.

Ofisi ya Mufti wa Zanzibar imewataka wataalamu wa Tiba Asili wanaotumia dawa za Kisuna na aya za Qur an kujisajili katika Ofisi hiyo ili kufanya kazi zao kwa misingi inayokubalika bila kuvunja Utamaduni na Silka za Zanzibar.

Hayo ameyasema  Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume wakati alipokuwa akizungumza na wadau wa Tiba Asilia Ofisini kwake Mazizini  kwa  lengo la kuwatambua na kufahamu sehemu wanaofanyia kazi zao.

Amesema Ofisi yake inahaki ya kusimamia shughuli zote zinazofanywa katika kusomea watu dua, ruqya pamoja na kutowa dawa za kisuna kwani imebainika zinafanywa bila kufuata utaratibu.

"Nataka  utaratibu ufuatwe mjisajili ili muweze kufanya kazi zenu kwa ufanisikatika kufanya visomo", alisema Katibu wa Mufti huyo.

Aidha amesema ofisi ya Mufti inapaswa kujua idadi ya waganga wanaotoa dawa za Kisuna Zanzibar, shughuli zao na kuwashauri kufata utaratibu na  nidhamu wakati wa kufanya kazi zao.

Pia amevitaka vyombo vya habari kutowaruhusu waganga wa dawa za kisuna kutoa matangazo ndani ya radio zao mpaka wawe wamesajiliwe rasmi vyenginevyo vinaweza kufungiwa.

Mkurugenzi Utawala, Mipango na Rasilimali watu Othman Mohamed Saleh amesema suala la kusoma dua limekuwa na mtihani mkubwa hivi sasa hivyo bila ya ujisajili hakutoweza kuwa na ufanisi mzuri.

Amesema makosa mengi yanayaona na sisi kama wahusika wa kusimamia masuala haya hatuwezi kunyamaza kwani tukikaa kimya kesho kwa Mungu tutakwenda kuulizwa.

Wakitoa michango yao waganga wa dawa za kisuna wamesema wako tayari kufuata utaratibu pamoja na nidhamu zilowewekwa na Ofisi ya Mufti na kuacha kuoneana choyo na watajenga mashirikiano katika kuwasaidia wananchi na kumuogopa Mungu.

Wakati huo huo Katibu wa  Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume amelaani vikali kitendo kilichofanywa na msanii Afande Suleiman wa Tanzania kwa kitendo alichofanya cha kutoa maneno ya kumtukana Mungu kwani maneno hayo yanaweweza kuvunja amani.

Amesema msanii huyo amevuka mipaka na kujisahau kama yeye ni binaadamu anastahiki kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa dini yeyote hivyo anamuomba atubu kwa mola wake kabla adhabu haijamfikia.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.