Habari za Punde

ZURA yafanya mabadiliko bei za mafuta

 Mwashungi Tahir                Maelezo                             7/3/2021.

Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imefanya mabadiliko ya bei za mafuta zitakazoanza kutumika rasmi kuanzia kesho siku ya Jumatatu ya tarehe 08/03/2021.

Akizungumza na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Zura ulioko Maisara Mkuu wa kitengo cha uhusiano wa Mamlaka wa Udhibiti na Maji na Nishati Zanzibar Mbaraka Hassan Haji wakati alipokuwa akiwasilisha  mabadiliko ya bei za mafuta.

Amesema ZURA inapanga bei kwa kuzingatiya mambo yafuatayo ikiwemo wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya  bei za mafuta Duniani (Platts Quatations )katika mwezi wa Febuary 2021, kwa lengo la kupata kianzio cha kufanya mabadiliko ya bei za mafuta kwa Mwezi Machi 2021.

Pia inaziingatia gharama za uingizaji wa mafuta katika Bandari ya Dar es slaam . Thamani ya shilingi ya Tanzania kwa Dola ya Kimarekani, gharama za usafiri , Bima na ‘Premium’hadi Zanzibar, kodi za Serikali na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.

Hivyo amesema bei zote za mafuta ya Petroli, Diseli na Mafuta ya Taa katika mwezi wa Machi 2021` zimeongezejka ukilinganisha na mwezi wa February 2021 kutokana na kubadilika kwa wastani wa bei na uuzaji wa bidhaa hizo katika soko la dunia pamoja na soko la ndani kwa kupitia bandari ya Dar es salaam.

Aidha amesema kwa upande wa aina ya mafuta Petroli bei ya mwezi wa February , 2021TZS /Lita 1,934, bei ya Mwezi wa Machi , 2021 TZS  LITA 2, 026 ambapo tofauti TZS 92 sawa na asilimia 4.76%.

Amesema aina ya mafuta ya Diseli bei ya mwezi wa February , 2021 TZS LITA 1,960 kwa upande wa Mwezi wa Machi , 2021 TZS LITA 2,041, tofauti TZS 81 sawa na asilimia 4.13%.

Kwa upande wa mafuta ya Taa bei ya mwezi wa February , 2021 TZS LITA1,376 kwa  Mwezi wa  Machi , 2021 TZS LITA 1,471 tofauti 95 sawa na asilimia 6.46%.

Kwa hiyo amesema ZURA inapenda kuwajuilisha wananchi kuwa bei zilizotangazwa ndio bei halali zitakazoanza kutumika kuanzia siku ya Jumatatu na amewaomba wananchi wanaponunuwa mafuta kudai risiti ili kunusuru usumbufu usije ukatokea katika vyombo vyao.

Vile vile amewaomba wenye vyombo vya usafiri kuacha tabia ya kutia mafuta wakiwa ndani ya magari wamepakia abiria kwa lengo la kuepuka athari yeyote itakayoweza kutokea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.