Habari za Punde

Mhe.Waziri Jafo Amefanya Ziara ya Kustukiza Kutembelea Katika Eneo la Swaswa Jijini Dodoma.

 

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph akimpa maelezo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo kuhusu mradi wa mabwawa ya maji taka katika eneo la Swaswa jijini Dodoma alipofanya ziara ya kushtukiza.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akikagua mabwawa ya maji taka katika maeneo ya Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua mazingira ya mabwawa hayo Aprili 29, 2021.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo ameipa wiki moja Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) kuomba Cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) katika mradi wa ujenzi wa mabwawa ya maji taka yanayotarajiwa kujengwa katika eneo la Nzuguni jijini humo.

Mhe.Jafo ametoa maelekezo hayo leo Aprili 29, 2021 alipofanya ziara ya kushtukiza katika mabwawa maeneo ya Hospitali ya Benjamin Mkapa na Swaswa jijini humo kukagua udhibiti wa maji taka.

Alisema kabla ya kuanza kujenga mradi wowote ni lazima kuanza mchakato wa kupata cheti cha TAM ambacho kinatoa mwongozo wa namna ya kujenga mradi huo.

“Mkurugenzi haya mabwawa ni sensitive sana kwa maisha ya watu sasa nitoe maelekezo muwasiliane na NEMC (Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira) tena wako hapa Dodoma anzeni mchakato wa kupata cheti na mtoe ushauri mbali ni changamoto na njia za kutatua kuhusu ujenzi huu,” alisema Jafo.

“Alhamisi ijayo niwaone tayari mmeanza mchakato na uzuri kila kitu kipo kwenye mfumo na nimetoa maelekezo, utaratibu wa kupata cheti usichelewe na ndiyo maana zaidi ya maombi 862 ya vyeti yamekuja na vyeti 30 vingine tayari vimeshatolewa,” aliongeza.

Pia aliitaka DUWASA kuanza mara moja ujenzi wa mabwawa katika eneo jipya la Nzuguni kwa kuwa eneo la Swaswa yalipo mabwawa hayo ni eneo la makazi na hivyo kuleta kero kwa wananchi wanaozunguka.

Hata hivyo alimpongeza Mkurugenzi wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph kwa kuwa na mikakati mizuri katika usimamizi wa maji taka na kumuahidi kuzungumza na mawaziri wenye dhamana ya Fedha na Mipango pamoja na Maji ili kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa haraka ili ujenzi uanze haraka iwezekanavyo.

AidhawazirihuyoalioneshakutoridhishwanaudhibitiwamajitakakatikamabwawayaliyopoHospitaliya Benjamin Mkapaambapopia alitoa wiki mojakwauongoziwa DUWASA kuboreshaeneohiloilikulindaafyazawananchi.

“Sijaridhikanahalinayoioanahapahuuuchafuunaovujakatikachembahiikamamvuakubwaikinyeshaunaewezakutiririkakwenyevyanzovyamajinakuletaatharizakiafyakwawananchi, name siwezikuvumiliakunawananchiwanaathirikasasa wiki mojahapapatengenezwe,” alisemaJafo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.