Habari za Punde

Maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi Mwaka 2021 Yakamilika Jijini Mwanza.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe Jenista Mhagama muonekano wa uwanja wa CCM Kirumba utavyokuwa, wakati wa kukagua maandalizi ya kuelekea sherehe za Wafanyakazi za Mei Mosi Jijini Mwanza, ukahuzi huo ulifanyika tarehe 29 Aprili, 2021..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza kuhusu masuala ya wafanyakazi wakati wa kikao kazi za maandalizi ya kufikia sherehe za Mei Mosi yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Kikao kilifanyika  tarehe 29 Aprili, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa huo.Kauli Mbiu ya Mei Mosi 2021: “Masilahi Bora, Mishahara Juu, Kazi iendelee”
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akieleza namna mkoa wake ulivyojipanga kufanikisha Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi, wakati wa kikao kazi cha Kamati ya Maandalizi hayo.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akizungumza wakati wa kikao cha Maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi Mkoani Mwanza.
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho wakifuatili maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Hayupo pichani)
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho wakifuatili maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Hayupo pichani)
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Prof. Jamal Katundu pamoja na wajumbe wa kikao cha Kamati ya maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi wakifuatilia kikao hicho.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.