Habari za Punde

NMB yakabidhi zawadi kwa mshindi wa Bonge la Mpango

Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (katikati) akimkabidhi  mshindi zawadi ya pikipiki ya magurudumu matatu - Paulina Moshi ,mkazi wa mtaa wa ujenzi Halmashauri Mbulu Mkoani Manyara. NMB ilimkabidhi mshindi huyo wa kampeni ya Bonge la Mpango inayoendeshwa nchi nzima kwa wateja wanaofungua au kuweka fedha kwenye akaunti zao za NMB. Kushoto ni Meneja wa NMB tawi la Mbulu, Rogate Iranga.

Mshindi wa kampeni ya Bonge la Mpango,Paulina Moshi akifurahia pamoja na Wafanyakazi wa Benki ya NMB baada ya kuifikisha pikipiki hiyo aliyoshinda hadi nyumbani kwake hapo.

Mshindi wa Bonge la Mpango, Paulina Moshi Mkazi wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara (mwenye tisheti yenye rangi ya chungwa) akishangilia pamoja na familia yake mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya pikipiki ya magurudumu matatu kwenya hafla iliyofanyika Tawi la NMB Mbulu.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.