Mwanasheria wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Lupakisyo Mwambinga akifanya ukaguzi wa kazi zinzazozalishwa na moja ya Ofisi za Kariakoo iliyopo Mtaa wa Aggrey uzalishaji wa kazi za Muziki na Filamu na kuwakuta wakidurufu za Muziki wa Bongo Fleva na Filamu za nje bila ya kuwa mikataba au makubaliano ya wamiliki wa kazi hizo, Operesheni hiyo ya ukaguzi imefanyika mei 18,2021 Jijini Dar es Salaam.
Mtuhumiwa wa Uzalishaji na Udurufu wa Kazi za Muziki na Filamu bila ya kuwa na kibali cha mmiliki wa kazi aliyekutwa akidurufu collection ya nyimbo za Muziki wa Bongo Fleva katika Ofisi yake iliyopo Kariakoo Mtaa wa Aggrey Bw.Ramadhan Sadiq akihojiwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukamatwa katika Operesheni ya Ukaguzi wa Hakimiliki iliyofanywa na COSOTA Mei 18, 2021, Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Mtuhumiwa wa Uzalishaji na
Udurufu wa Kazi za Muziki na Filamu bila ya kuwa na kibali cha mmiliki wa kazi
aliyekutwa akidurufu Filamu za Nje ya nchi katika Ofisi yake iliyopo Kariakoo Bw.Frank
Manyama ambaye ni Msimamizi wa Sanyiwa Production akihojiwa na waandishi wa habari (hawapo
pichani) mara baada ya kukamatwa katika Operesheni ya Ukaguzi wa Hakimiliki iliyofanywa
na COSOTA Mei 18, 2021, Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Na Anitha Jonas – COSOTA,Dar es Salaam.19/05/2021
Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imefanya operesheni
katika baadhi ya maeneo ya uzalishaji wa kazi za Filamu na Muziki na ambapo
kukamata zaidi ya mashine 50 zenye uwezo wa kudurufu takribani nakala 10,000
kwa nusu saa.
Operesheni hiyo ya uharamia wa kazi za Muziki na Filamu imefanyika
Mei 18, 2021 Kariakoo, Jijini Dar es Salaam ambapo takribani watuhumiwa kumi na moja wanafanya
shughuli za uazalishaji wa kazi haramu za filamu na Muziki walikamatwa na kufikishwa
Kituo cha Polisi Msimbazi kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.
Akizungumza katika Operesheni hiyo Mwanasheria wa COSOTA
Bw.Lupakisyo Mwambinga alieleza kuwa suala uharamia wa kazi za Muziki na Filamu
umekithiri nchini hivyo COSOTA imedhamiria kukomesha hilo kwa kufanya
operesheni endelevu za kukamata kazi zote nje na ndani ambazo zinazalishwa bila
kufuata sheria.
"Kifungu cha 42 cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki kamakilivyofanyiwa
marekebisho na Sheria namba 3 ya mwaka 2019 kinasema ukikamatwa kwa kosa la
uvunjifu wa Hakimiliki faini yake ni isiyopungua milioni ishirini au
Kifungo cha Miezi sita na kisichozidi Miaka Mitatu au vyote kwa
pamoja,"alisema Bw.Mwambinga.
Pamoja hayo Mwanasheria huyo alitoa onyo kali kwa wazalishaji
wote na wasambazaji wa kazi za Muziki na Filamu ambao wanaburn CD za Muziki na
Filamu, wanaoweka Muziki kwenye flash kwa kusema kuwa hilo ni kosa, na alisisitiza
kuwa COSOTA imedhamiria tutahakikisha
tunathibiti hilo na kwa yoyote atakayekamatwa na kazi hizo zisizo na mikataba
au makubaliano na wamiliki atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Halikadhalika Bw.Mwambinga alifafanua kuhusu udurufu wa
Filamu za nje bila kufuata utaratibu kuwa ni kosa na aliwasihi
wazalishaji hao kuachakudanganyana, kwa kusema udurufu au uzalishaji wa kazi
za nje bila kibali cha mmiliki unaruhusiwa,hivyo
alisisitiza katika uuzalisha au udurufu wa kazi yoyote iwe Muziki au Filamu ya
ndani au ya nje ya nchi ni lazima kuhakikisha kuwa unamakubaliano au mikataba
na mmiliki wa kazi hiyo kinyume na hapo huo ni uharamia na uvunjifu wa Sheria
ya Hakimiliki.
Kwa upande wa Mtuhumiwa wa Uazilishaji ambaye ni Msimamizi wa Kampuni
ya Sanyiwa Production Bw.Frank Manyama alikiri kufanya kosa la kuzalisha kazi
mbalimbali za ndani na nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha wamiliki wa kazi
hizo.
Operesheni hiyo sehemu ya majukumu ya COSOTA katika kulinda
Hakimiliki za Wasanii. na kazi zote za ubunifu.
No comments:
Post a Comment