Habari za Punde

SMZ Itaendelea Kuifuatilia kwa Karibu Mipango ya Maendeleo ya Jamii Tasaf na Mkurubita Ili Kuhakikisha Inawanufaisha Wananchi.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Tanzania  ukiongozwa na Waziri wa wizara hiyo (MB) Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk. Hussein Ali Mwinyiamesema kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuifuatilia kwa karibu mipango ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)ili kuhakikisha inawanufaisha wananchi walio wengi hapa nchini.

Rais  Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo, Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohamed Omary Mchengerwa, akiwa na ujumbe wake wa viongozi wanaosimamia masuala ya TASAF, MKURABITA na Ajira katika Utumishi wa Umma waliofikaIkulu kwa ajili ya kujitambulisha.

Katika maelezo yake, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa kwa vile Zanzibar ni ndogo ikilinganishwa na Tanzania Bara anaimani kwamba mafanikio zaidi ya Mipango ya TASAF na MKURABITA yatafikiwa kwa haraka zaidi.

Alisisitiza haja ya changamoto zilizokuwepo kufanyiwa kazi sambamba na  mafanikio yaliopo kuelezwa ili yajulikane.

Kwa upande wa ajira Rais Dk. Mwinyi alitoa shukurani kwa Waziri huyo kwa jinsi anavyolifuatailia suala hilo na kumpongeza huku akimtaka kuendelea kuhakikisha mafanikio zaidi yanapatikana kutokana na taratibu zilizoanza kuwepo.

Rais Dk. Mwinyi alieleza haja kwa Zanzibar kujifunza kutoka Tanzania Bara jinsi wanavyofuatilia shughuli hizo pamoja na taratibu za kufanya usaili pamoja na kuwa na danzi data za kutosha haliambayo inapunguza usumbufu kwa wanaoomba ajira.

Alisema kuwa utaratibu mpya uliopangwa ana matumaini makubwa kwamba utaleta mafanikio makubwa na kusisitiza haja ya kubadilishana uzoefu hatua ambayo itapelekea pande zote mbili za Muungano kufanikiwa.

Rais Dk. Mwinyi alipongezahatua zilizofikiwa ikiwa ni pamoja na jinsi ya mgawanyo wa mkopo wa fedha unavyofanyika katika mipango ya TASAF sambamba na hatua zinazochukuliwa katika MKURABITA na kueleza jinsi mashirikiano mazuri yaliyopo.

Mapema Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mohamed Omary Mchengerwa alimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba Wizara yake imekusudia kutekeleza malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yale yaliyokusudiwa katika Katiba yanafanyiwa kazi kwa vitendo.

Alieleza mafanikio yaliyopatikana katika  miradi ya TASAF kwa upande wa Zanzibar huku akieleza namna ya mgao wa ajira unavyofanyika na kueleza changamoto zilizopo katika suala la ajira na namna zinavyofanyiwa kazi hivi sasa .

Alisema kuwa kuanzia sasa Wizara hiyo itakwenda sambamba katika michakato yote ya ajira ili kwa upande wa Zanzibar zifahamike pamoja na ushiriki mzuri uwepo.

Alisema kuwa kwa upande wa Zanzibar katika masuala ya TASAF yameenda vizuri na kueleza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuhakikisha kwamba Kaya zote hapa nchini zimefikiwa kwa azma ya kila Mtanzania aweze kufikiwa.

Aidha, Waziri Mchengewra aliipokea rai ya Rais Dk. Mwinyi ya kutaka kupatikane kwa mafunzo sambamba na kubadilishana uzoefu kwa watendaji katika masuala ya ajira na  utulimishi wa Umma kutoka Zanzibar kwenda kujifuza Tanzania Bara.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ladislaus Mwamanga  alisema kuwa Mfuko huo ulianzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2000 kama mojawapo ya mikakati ya Serikali katika kupambana na umasikini kwa kutumia dhana ya ushirikishaji jamii na kutatua kero zao.

Alisema kuwa awamu ya kwanza  ya TASAF, umetekelezwa katika maeneo 42 zikiwemo Halmashauri 40 za Tanzania Bara na Zanzibar na kutekelezwa kwa mafanikio makubwa katika huduma za elimu, maji, afya na nyenginezo ambapo jumla ya iradi 1,704 yenye thamansi ya TZS Bilioni 72 ilitekelezwa.

Aliongeza kuwa utekeleza jiwa TASAF Awamu ya Pili ulifanyika kwa kipindi cha miaka minane kuanzia mwaka 2005 hadi 2013 na jumla ya miradi 12,347 katika sekta mbali mbali yenye thamani ya TZS Bilioni 430 ilitekelezwa kwa ajili ya kutatua kero za wananchi.

Alisema kuwa katika Awamu ya Tatu ya TASAF ambayo ilipangwa kutekelezwa kwa miaka 10 yenye vipindi viwili viwili ambapo jumla ya TZS Bilioni 430 zilitumika.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa kipindi cha kwanza kilihusisha Vijiji, Mitaa na Shehia 9,960 ambazo ni silimia 70 zilifikiwa na asilimia 30 zilizobaki zitafikiwa katika kipindi cha Pili ambacho kinatarajiwa kumalizika Julai 2021 na kutumia trilioni 2.03.

Kwa upande wa Zanzibar alisema kuwa miradi 75 yenye thamani ya TZS Bilioni 3.0 ilitekelezwa katika awamu ya kwanza na awamu ya Pili miradi 814 yenye thamani ya TZS Bilioni 8.8 ilitekelezwa katika kipindi cha kwanza cha Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Mpango ambapo Shehia 204 zilitekeleza miradi ya TZS Bilioni 45 na kwa kipindi cha Pili utekelezaji ndio umeanza na Bilioni 112.87 zimetengwa kwa Wilaya zote na Shehia za Zanzibar kwa miaka minne ijayo mpaka 2023.

Nae Xavier Daud,  Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma alieleza majukumu ya Sekretarieti hiyo huku akieleza jinsi ya vikao vya pamoja vinavyokaliwa ambapo kikao cha Aprili 21, 2011 kilieleza namna ya kutatua changamoto za Muungano hususan eneo la Ajira katika Utumishi wa Umma.

Alieleza kwamba katika vikao hivyo ilikubalika kuwe na uwioanio wa Ajira kwa taasisi za Muungano ambapo ilikubalika kuwa Tanzania Bara iwe na asilimia 79 na Tanzania Zanzibar iwe na asilimia 21 ya nafasi za ajira kila zitakapotangwazwa.

Katibu huyo alitoa shukurani kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwapatia Ofisi yenye dhamana na Utumishi wa Umma Zanzibar ajira zipatazo 92 zilitolewa kwa Wazanzibari ambapo kwa Taasisi za Muungano ni 42 na Taasisi binafsi ni 50 kuanzia Julai 2015 hadi Machi 2021.

Dk.Seraphia Mgembe Mkurugenzi Mkuu MKURABITA alieleza shughuli ilizozitekeleza ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo kwa ajili ya urasimishaji wa ardhi vijijini ambapo kwa upande wa Zanzibar viwanja 4,600 vimepimwa na hati za matumizi ya ardhi 116 zimetolewa na zinaendelea kuandaliwa.

Alieleza shughuli nyengine ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa urasimishaji wa biashara, kuwajenga uwezowananchi wa namna ya kutumia hati miliki za rasilimali walizorasimisha.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.