Habari za Punde

Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani Kwa Kufanya Kongamano.

Na Rahma KhamiS Maelezo                          10/5/2021

Jumla ya wagonjwa 1074 wa maradhi ya Kifua Kikuu (TB) wameripotiwa mwaka jana katika jamii baada ya uchunguzi uliofanywa na Programu shirikishi ukimwi, homa ya ini, kifua Kuu na ukoma Zanzibar.

Hayo yameelezwa na Mkufunzi Dkt Julius Obed katika Ukumbi wa Chuo cha Afya Mbweni wakati akitoa mafunzo katika Kongamano la Siku ya TB duniani lilowashirikisha wanafunzi wa kada mbalimbali katika Skuli ya Afya Mbweni.

Amesema idadi hiyo imeongezeka kutokana na baadhi ya wagonjwa wa zamani  kujirejea tena maradhi  hayo na kuifanya idadi hiyo kuwa kubwa na kupelekea wasiwasi katika jamiii.

Amesema  kuwa Zanzibar  mwaka 2012-2013 idadi ya wagonjwa 989 hadi kufikia mwaka 2020 wameongezeka sawa na asilimia 92 ambao ni wagonjwa hao ni wapya.

Aidha amefahamisha  kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wa maradhi hayo inatoka mjini na kwa upande wa Pemba inaongoza katika Wilaya ya Chakechake hivyo ipo haja kwa wahusika kuwafikia zaidi watu wa vijijini ili kupata idadi ya wagonjwa waliyoko huko.

Akifungua kongamano hilo Kaimu Meneja wa kitengo Shirikishi ambae pia ni Mwenyekiti  wa Kongamano hilo Issa Abeid Mussa amesema kuwa lengo la kuadhimisha siku ya Tb Duniani ni kukumbuka ugunduzi wa bektiria mwaka 1982 anaesababisha maradhi hayo na pamoja na kuwapa taaluma wanafunzi ili kuibua wagonjwa.

Amesema siku hiyo hiyo ili kuielewesha jamii kutambaua uwepo wa maradhi ya TB na namna ya kujikinga kutokana na jamii kubwa kukosa uwelewa wa maradhi hayo.

Maadhimisho hayo huadhimishwa kila ifikapo mach 24 ambapo kwa mwaka huu wamefanya Machi 10 kutokana na kifo cha cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kaimu Issa amefahamisha kuwa katika mafunzo yao pia wanashughulikia maradhi ya mripulko ili kupambana nayo hivyo  jitihada zaidi zinahitajika ili kuondosha kabisa maradhi ya TB ifikapo mwaka 2030.

Nae Mwakilishi kutoka WHO Dkt VendelinSimon amesema kuwa vita vya maradhi ya kifua kikuu ni lazima kila mtu kichukua juhudi ya kupambana nayo kuanzia familia na jamii kwa ujumla.

Aidha  amezitaka Taasisi husika kushirikiana kwa pamoja na kuunda timu  shirikishi na kutoa kazi ya kwa kufuatilia kazi katika maeneo ya vijini  ili kuweza kutambua jinsi gani TB inapatikana na namna gani ya kujikinga na maradhi hayo.

Nao washiriki katika kongamano hilo wameiomba Wizara ya Afya kupitia kitengo shirikishi cha maradhi ya Ini,Ukoma Ukimwi na TB kufuatilia wagonjwa wa maradhi hayo majumbani ili kupambana na kudhibiti maradhi hayo yasienee katika jamii.

Katika kongamano hilo mada mbili zimejadiliwa, jinsi gani tutatambua wagonjwa Zanzibar na vipi Tasisi za elimu ya vyuo vikuu vitatokomeza TB ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni MUDA UNAPITA TUONGEZE MAPAMBANO DHIDI YA KIFUA KIKUU.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.