Habari za Punde

Wadau wa Habari Zanzibar Wajadili Mabadiliko ya Sheria ya Habari Zanzibar.

Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa mabadiliko ya Sheria ya Habari Zanzibar wakijadiliana kuhusiana na mabadiliko hayo uliofanyika katika ukumbi wa Malaria Mwanakwewrekwe Jijini Zanzibar.

Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa amesema kuna umhimu mkubwa wa madiliko ya sheria ya habari Zanzibar kwani  uwepo wa sheria bora ni chachu ya maendeleo na kivutio kikubwa kwenye sekta ya uwekezaji.

Aliyasema hayo leo katika mkutano maalumu uliowashirikisha wadau mbali mbali wa habari wenye lengo la kujadili rasimu ya sheria ya hio visiwani hapa uliofanyika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe mjini Unguja.

Alisema  kwa miaka mingi Zanzibar imekua na sheria ya habari isiolingana na wakati uliopo sasa na kupelekea changamoto mbali mbali ambazo ili ziweze kuondoka ni lazima iwepo sheria mpya na yenye kukidhi maakwa ya wadau wa sheria hio kwa kuwa ndio wenye kufahamu kwa kina nini kinachohitajika na kisichopaswa kuwepo kwa wakati uliopo sasa.

Akifafanua zaidi alisema kwa sasa sheria nyingi za habari zilizopo zimepitwa na wakati na hakuna budi lazima mamlaka kubadilisa sheria hizo kwa manufaa ya pande zote.


Mkurugenzi huyo alieleza kuwa kutokuwepo kwa mazingira bora ya sheria ya habari kupelekea tasnia hio kuonekana kutokua bora wakati tasnia ya habari ni muhimu sana popote pale duniani.

Akifafanua zaidi alisema kuwepo kwa mazingira magumu ya sheria ndio maana baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikifungiwa ovyo bila ya kuelezwa sabau za msingi za kufunggiwa kwake jambo ambalo anaamini kutwepo kwa sheria mpya kutaondokana na kadhia za ina hio.

Katika hatua nyengine alisema wadau wa sekta ya habari Zanzibar wanawajibu wa kutafakari kwa kina na kuhakikisha wanachangia kwa kiasi kikubwa  upatikanaji wa sheria mpya itakayokidhi vigenzo vyote.

Kwa upande wake mwandishi wa habari na mkufunzi wa taaluma hio Rashid Omar amesema upatikanaji wa sheria mpya ya habari ni matakwa ya wadau wengi Zanzibar na wakati umefika kuzingatiwa kwa matakwa hayo.

Nae Shifaa Sadi Hassan mwakilishi wa Baraza la Habari Tanzania MCT ofisi ya Zanzibar alisema hadi leo hii Zanzibar haina sheria mahsusi ya habari yenye kukidhi vigenzo na hadi sasa imekua ikitumika sheria ya mwaka 1988 inayogusia kwa uchache sana kuhusu sekta ya habari.

Alisema kwa kuwa suala la  kukuza na kueneza habari ni jambo  muhimu linalopaswa kuungwa mkono na kila mtu kwani ni haki ya kikatiba ambayo inapaswa kuzingatia ikiwemo kupata sheria bora.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.