Habari za Punde

Waziri Bashungwa Amtembelea Msanii wa Muziki wa Dansi Nchini Tanzania Kikumbi Mpango.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amemtembelea Msanii Mkongwe wa Muziki wa Dansi nchini Tanzania Kikumbi M. Mpango almaarufu King Kikii Muimbaji wa nyimbo Maarufu ya Kitambaa Cheupe Nyumbani kwake Mtoni Kwa Azizi Ali Jijini Dar es Salaam Leo 22 Mei 2021.

Waziri Bashungwa akiwa ameongozana na Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Ndugu Matiko Simoni Mniko Wamefika nyumbani kwa Nguli huyo wa Muziki ili kumjulia hali kutokana na Ugonjwa wa Miguu unaomsumbua kwa Muda mrefu.

Waziri Bashungwa amemtia moyo na na kumsihi azingatie sana mazoezi na matibabu kwakuwa Serikali chini ya Wizara wanafuatilia katibu Maendeleo yake na Matibabu kwa ujumla.

“wizara itaendlea kufuatilia kwa ukaribu matibabu yake na kwasababu daktari wake tunamawasiliano ya ukaribu tutakuwa tunajua hali yake inavyoendelea kila siku.”

Vile vile waziri anawahimiza wasanii wote kukata bima ya afya pindi wakiwa na kipato na nguvu kwakuwa hali ya afya huwa haitabiliki muda wote hasa ukiwa umejiajiri wewe mwenyewe

Nae King Kikii amemshukuru Waziri Bashungwa kwa Kumtembelea na kumfariji pia akamuomba Waziri amfikishie Salam zake kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakumpongeza kwa kazi yake nzuri yakuliongoza Taifa.

Vile vile King Kikii ameongeza kwa kuwahasa wanamziki hasa vijana kuwa na nidhamu katika kazi na kuachana na maisha ya starehe zisizo za masinga kama pombe ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa utendaji mzuri wa kazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.